January 13, 2017

Siri 7 zitakazomfanya umpendaye 'Mke' awe na furaha siku zote.

1. Umshtushe mke wako siku moja na mandari (mtoko). 
Panga mahali pa kukutania siku za wikiendi au siku yoyote ambapo mna siku ya mapumziko. Hakikisha kuwa hana ratiba yoyote nyingine zaidi ya hiyo. Ndipo unapomwambia kuwa aambatane na wewe mwende kwenye supermarket au kitu kifananacho na hiki. Mpe muda wa kujiandaa vizuri, muda wa kuingia kwenye gari, na munaweza kubeba hata vyakula laini ama vipoza njaa. Mpeleke mwenzi wako kwenye bustani nzuuri maarufu kama beach na mwambie kuwa unampenda na ndiyo maana umeeandaa hili tukio ili kumdhihirishia ni jinsi gani unampenda.

2. Mwandikie mashairi. 
Na kama hii sio hobi yako pia zipo sehemu nyingi zenye mvuto. Jaribu kumsomea kitabu cha mashahiri yenye ujumbe wa kumsifia, nyimbo za upendo n.k. usirudie neno lolote kwasababu itazoeleka na atakudharau.

3.  Mpikie chakula kizuri na kitamu, washa mishumaa punguza mwanga wa taa na safisha nyumba. Na atakapofika nyumbani atakosa cha kusema.

4. Shika mkono wake kila mara mnapokwenda mahali popote nje na nyumbani. Kama hili haliwezekani {kwasababu mmoja wenu amebeba mototo} hakikisha unaendeleza mawasiliano ya nje. Hii itamfanya ajisikie kuwa unajivunia ukiwa nae na kamwe huwezi kumuacha.

5. Panga ratiba ya kupiga picha. 
Mpe nafasi mke wako ama rafiki wako wa kike ajipambe kwaajili yako, pia chukua picha zake ambazo utaweka kwenye pochi yako, ofisini ama kwenye gari lako. Mwambie kwamba yeye ni mzuri na kuwa amepiga picha nzuri.

6. Pata muda mchache wa kwake siku moja na umwandikie neno rahisi tu “Nakupenda” na bandika popote pale. Bandika hilo neno bafuni kwenye kioo ama sehemu ambao kwa haikka ataona huo ujumbe. Hii huimarisha na kumfanya yeye kuwa wa pekee sana kwako na kukupenda sana. Na kama unahitaji kupanua wazo hili unaweza kumuachia ujumbe mtamu katika maeneo yake machache pale unapotoka.

7. Kama wewe ni mchoraji unaweza ukapata hamasa na kuchora Titanic, ukapaka rangi ama kumchora umpendaye. Utapata majibu mazuri kama amani yako imeimarishwa na kama bado mwambie kwamba huwezi kuumba kitu kizuri sana kama wewe.

By Chief Hope 

Jiunge Na Tim Heaven Sasa! 
Kupitia FacebookTwitterInstagram ili kupata habari, makala juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.