Featured Posts

January 26, 2017

Mambo 3 muhimu unayohitaji ili kukamilisha malengo yako.

1. Dira.
Dira hukupa uelekeo wa wapi unataka kwenda. Jaribu kukaa na kufikiria unataka nini? Fikiria Mafanikio /Mambo mazuri ambayo wewe unayataka. Ni wewe mwenyewe ndio una mtazamo sahihi wa maisha yako na ni wewe mwenyewe ndio unatakiwa kusimama Imara kwa ajili ya kutetea kile unachokitaka wewe.

 2. Ndoto. 
Ukiwa na Ndoto za kufika mbali lazima uwe makini ktk fikra unazofikiria. Lazima uwe na Positive view kuhusu Ndoto zako. Ukifikiria vibaya na matokeo huweza kuwa mabaya vile vile.. Ukifikiria vizuri na kuamua kuchukua uamuzi mzuri lazima uone matokeo mazuri pia.

3. Sikiliza Nafsi.
Jaribu kutumia muda wako wa ziada angalau dk 3-5 jiulize wewe mwenyewe je, Unataka nn au unahitaji nini ambacho kinaweza kukusaidia kubadili maisha yako kwa namna moja au zaidi. Ukipata jibu tafakari na uchukue hatua nzuri.

Mwalimu Adson whatsapp 0756508071.