January 3, 2017

Mchungaji Lusekelo 'Mzee wa Upako' 'kufungua kituo cha televisheni.

NEMchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo amesema ana mpango wa kufungua kituo cha televisheni ili aachane na kulipia vipindi katika vituo vingine

Akitoa mahubiri ya Mwaka Mpya kanisani kwake Ubungo jijini hapa, Lusekelo maarufu kwa jina la Mzee wa Upako amesema: "Haya ni mafanikio ambayo yanakuja licha ya kupigwa vijembe na magazeti."

Hata hivyo, amesema kumekuwa na vita ya maneno kwenye vyombo vya habari lakini havitashinda.

Mchungaji huyo amekuwa katika malumbano na vyombo vya habari baada ya kuripoti habari kwamba aliwafanyia fujo majirani zake akiwa amelewa na tukio hilo kuripotiwa katika Kituo cha Polisi cha Kawe.

By Chief Hope

Jiunge Na Tim Heaven Sasa!
 

Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter na instagram ili kupata habari mbalimbali juu ya muziki, mahusiano, mafanikio afya nk.