January 17, 2017

Kilichompata Pastor aliyetabiri kifo cha Rais Robert Mugabe.

Kama unakumbuka mwishoni mwa mwaka 2016, raia na wafuasi wa vyama vya upinzani nchini Zimbabwe waliandamana kupinga utawala wa Rais Robert Mugabe ambaye amekuwa madarakani tangu 1980.

Habari zilizoripotiwa na vyombo vya habari vya kimataifa zimedai kuwa maafisa wa polisi nchini Zimbabwe wamemkamata na kumzuilia mhubiri aliyetabiri kwamba Rais Robert Mugabe atafariki mwezi Oktoba mwaka huu.

Pasta Patrick Mugadza alikamatwa akiwa mahakamani mjini Harare Jumatatu ambapo alikuwa ameenda kwa kesi nyingine dhidi yake, wakili wake Gift Mtisi amewambia waandishi wa habari kuwa alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya kuvalia bendera ya taifa
Wakili wake ameimbia AFP kuwa "Alikuwa amefika mahakamani kwa kesi hiyo polisi walipomkamata wakati wa mapumziko na kumfungulia mashtaka kwa sababu ya unabii huo"
‘Awali alishtakiwa kwa kukosea heshima mamlaka ya Rais lakini shtaka hilo likabadilishwa baadaye na kuwa amewatusi watu wa asili fulani au dini fulani’.

Pastor Mugadza wiki iliyopita aliandaa kikao na wanahabari ambapo alitabiri kwamba Mugabe atafariki Oktober 17 mwaka huu.