January 28, 2017

Njia 5 za kumpenda mke wako kwa vitendo.

1. Hakuna kitu wanawake wanazimia kama kukumbatiwa na kupigwa busu mara kwa mara.
Kabla hujakurupuka kitandani hakikisha umemkumbatia na kumbusu hata kama kalala (hakuna raha kama kuamshwa na busu au mkumbatio).


Soma: Hizi Hapa Faidia Nne '4' Za Ndoa.


2. Mwambie jinsi gani unampenda na unavyopenda chapati, mayai, viazi alizopika au hata jinsi alivyoandaa mlo wa asubuhi.
Wakati unatoka ndani kumbatia chap-chap na busu kiduchu ndio utokomee kazini, hata kama mnatoka wote kwenda kwenye kituo cha daladala unafanya hivyo kabla hujakanyaga vumbi la nje baada ya kupata kifungua kinywa.

3. Onesha unajali kwa kumjulia hali kwa sms au sauti mara baada ya kufika kwenye mihangaiko yako na vilevile kumbuka kufanya hivyo kabla hujaondoka eneo la shughuli zako pia hakikisha unamueleza utakuwa saa ngapi nyumbani au kama kuna mahali unapitia basi mfahamishe utakuwa huko kwa muda gani.


Ufikapo nyumbani mkumbatie na busu la mdomoni sio shavuni, badala ya kukimbilia kusema yaliyojili huko utokako.

4. Mnunulie vijizawadi mara kwa mara, Wazaramo hununuliwa khanga au hereni na mikufu ya dhahabu, Wazungu hununuliwa maua, kadi au vidani vya madini tofauti, kuna wengine ukipeleka kitoweo (aina ya nyama) basi umemaliza kesi; mwanamama anafurahi kwelikweli sasa wewe fanya kile unachomudu sio kila siku wala kila mwezi.


Soma: Changamoto 6 Za Kuoa Mwanamke Aliyekuzidi Umri.


5. Msaidie kusafisha meza au jamvi mara baada ya mlo wa jioni, ikiwa umechoka hata yeye kachoka pia hivyo mkikutana nyumbani ‘mna-share’ kufanya usafi ili kuokoa muda.