January 27, 2017

Neno La Siku: Kabla yakushinda utashindwa tu - Job Mkama.

Nimejifunza kutambua kuwa watu wasio na mafanikio katika maisha ni wale wanaoogopa kushindwa! Hawa ni watu ambao hawana rekodi ya kushindwa katika maisha! Hawana rekodi ya kushindwa katika maisha kwa sababu hawana rekodi ya kujaribu kufanya kitu!

Watu wote wenye Mafanikio makubwa duniani ni wale waliojaribu kufanya mambo wakashindwa mara kadhaa katika majaribio yao kuliko yale waliyofanya yakafanikiwa.

Endekea kuogopa ili ubakie ulivyo!! - Job Mkama.