January 23, 2017

Sio kinyonga tu, kuna viumbe 10 wengine wanaoweza kubadili rangi zao kulingana na mazingira.

Uwezo wa kubadili rangi ya mwili kufanana na mazingira (camouflage) kwa baadhi ya viumbe duniani huwasaidia kujilinda dhidi ya maadui na pia katika kuwinda chakula chake. 

Kwa kuweza kubadilika huku, viumbe hivi huweza kuwa karibu kabisa na maadui zake au na windo lake bila kuonekana hivyo kumhakikishia usalama wake au kumrahishia kupata chakula.

Kuna viumbe wengi sana duniani wenye uwezo wa kubadilika rangi kufanana na mazingira anayokuwapo. Kwa sisi Watanzania, tumezoea kumuona kinyonga kwakuwa ndiye aliyepo kwenye mazingira yetu.

Zifuatazo ni picha 10 za viumbe wenye uwezo wa kufanya hivi:

1. Samaki Bapa (Stone Flounder)

2. Chavichavi aina ya Baron (Baron Caterpillar)
  
3. Bundi.

4. Mjusi aina ya Gecko.

5. Gecko mwenye mkia unaofanana na majani (Leaf-Tailed Gecko) 

6. Mdudu Fimbo (Stick Insect)

7. Chura.

 8. Buibui (Spider) 

9. Farasi wa Baharini (Seahorse)

10. Chui wa kwenye barafu (Snow Leopard)