January 20, 2017

Jinsi ya kuwa mbunifu katika ujasiriamali.

http://timheaven.blogspot.com/
Ni jambo lililo wazi kuwa sote tunakumbana na matatizo , ingawaje aina ya matatizo na kiwango ambacho yanatusumbua vinaweza kuwa tofauti.

Hata hivyo, sote tunaweza kutafuta mbinu za kutatua matatizo husika, ingawaje ni kweli mbinu zetu za kutafuta suluhu zinaweza kuwa tofauti.


Katika makala hii kutana na wabunifu Ed na Ross kutoka UK, wanaoendesha biashara yao iitwayo BUY MY FACE.

Ed na Ross kutoka UK
Vijana hawa walianzisha biashara ya kuuza nafasi za matangazo kwa kutumia sura zao. Wanachofanya ni kuandika tangazo kwa uso zao, kisha huzunguka maeneo tofauti tofauti ya mji ili watu waweze kuona tangazo husika.


Na wameshafanya matangazo ya makampuni makubwa kama vile Ernest & Young.


Mambo kadhaa yanayoweza kukufanya kuwa mbunifu:-

1. Ondoa uwoga: 

Usiogope kuwa wazo lako litakuja kushindwa. Chukulia kuwa hata kama litakuja kushindwa, utakuwa tayari umeshapata uzoefu wa kutengeneza wazo lingine bora zaidi.

2. Usijilinganishe na watu wengine:  

Usiangalie wengine unao dhani wamekuzidi uzoefu au ujuzi wamefanya nini , kiasi kwamba ukajishusha kuwa eti wewe hauwezi kufikia kuwa na kitu kizuri cha ubunifu.

3. Zingatia Upekee: 

Kama unataka kufanya UBUNIFU, lakini mawazoni mwako unapata ukinzani wa kutaka kufanya kama fulani, basi ujue hapo kuna tatizo. Sisitiza kuwa na upekee, na upekee tuu ndio utakaoleta maana haswa katika ubunifu wako, hata mbele za wateja. Hata hivyo hii haimaanishi kuwa hautakiwi kuangalia wengine wamefanya nini, hapana, angalia wengine kwa lengo la kujifunza, na kutambua mapungufu.

4. Zingatia kukidhi mahitaji ya binadamu:
  

Ubunifu wako hautokuwa na maana kama haukidhi mahitaji ya watu. Hivyo njia rahisi ya kuanza ubunifu ni kuisoma jamii, kuangalia matatizo yanayoikumba jamii. Sio lazima uangalie mbali sana, waweza hata kutafakari matatizo ambayo yamekuwa yakikutatiza wewe mwenyewe, kisha ukaamua kubuni kitu cha kuleta suluhisho. Fanya uchunguzi kujua wengine wamekumbana na matatizo kama yako.

Mfano mzuri, Drew Houston mwanzilishi wa huduma ya kuhifadhi documents online, DROPBOX anasema alianzisha huduma hiyo baada ya yeye mwenyewe kuwa mpotezaji wa flashdisk wakati akiwa chuoni MIT.