January 15, 2017

Vyakula 5 vinavyosaidia na vinavyosababisha tatizo la kukosa choo.


Kukosa choo ni tatizo kubwa katika jamii zetu japo huwa halionekani kama ni tatizo. Hata hivyo kuna vyakula ambavyo vinapatikana kwa urahisi na vinasaidia kutibu tatizo la kukosa choo kwa njia rahisi kabisa.


Kwa kawaida mtu mwenye afya njema anatakiwa kwenda chooni angalau mara tatu kwa siku,lakini si ajabu kusikia mtu hajaenda chooni siku tatu na tunaona ni kawaida sana kwenda chooni mara moja kwa siku.


Tatizo la kukosa choo (Constipation) linatokana na chakula tunachokula kuchelewa kuunguzwa tumboni hivyo kuchukua muda mrefu katika mfumo wa usagaji.


Baadhi Ya Vitu Vinavyosababisha Tatizo La Kukosa Choo:

 • Kutokunywa Maji ya Kutosha
 • Kutokula vyakula vyenye fiba kama matunda na mboga za majani
 • Ulaji wa nyama nyekundu kwa wingi
 • Unywaji wa maziwa kupita kiasi
 • Kutofanya kaziza kushughulisha mwili na kukosa mazoezi.

Vyakula Vinavyosaidia Kutibu Tatizo La Kukusa Choo
 • Tende
 • Maji
 • Kahawa Na Vinywaji Vingine Vya Moto
 • Ulaji Wa Matunda Au Saladi
 • Ulaji Wa Mboga Za Majani

Mazoezi Husaidia Kutibu Tatizo La Kukosa Choo Pia:

 • Ukiachia vyakula, ufanyaji mazoezi au kazi zinazoshughulisha mwili zinazaidia kuzuia na kutibu tatizo la kukosa choo. Kufanya mazoezi kila siku angalau kwa dakika 30 ni jambo linalowezekana kama utalipa muda na kuweka katika ratiba zako.
 • Mazoezi rahisi kabisa ni kukimbia (jogging) na pia hushughulisha mwili mzima(Total Body Exercise).