February 3, 2017

Neno La Siku: Unafanana na unachosikia - Job Mkama.

Maneno yana nguvu, maneno yana uzito, maneno yanalemea, na maneno ni roho. Maneno yanaweza kuwa uzima wako au mauti kwako! Jifunze kusikiliza vitu vinavyokujenga. Sikia sasa! Je wajua kuwa kile unachokiamini leo kimetokana na kile ulichosikia jana na hivyo ndivyo ulivyo sasa?? 

Siku njema! - Job Mkama.