February 1, 2017

Neno La Siku: Kwani shida ni nini? - Job Mkama.

Watu wana haki ya kukufikiria wewe vyovyote vile wanavyotaka wao ingawa hiyo inapaswa isikufanye wewe kuwa vile wanavyokudhania! Wewe ni wewe na kamwe usibadilishwe na mitazamo ya watu wengine! Usipokuwa makini utajikuta ukiishi maisha ya watu wengine badala ya kuishi maisha yako mwenyewe!
Yaishi maisha yako utimize ndoto zako kama unajipenda! Hukuzaliwa kumfurahisha kila MTU! Umezaliwa kwa jukumu maalumu!

Siku njema! - Job Mkama.