Featured Posts

March 21, 2017

Askofu Josephat Gwajima asema haya kuhusu Clouds Media.

Askofu Mkuu wa makanisa ya Ufufuo na Uzima, Dr. Josephat Gwajima kwenye akaunti yake ya Instagram ameandika taarifa ya kufanya ziara kwenda kutembelea ofisi za Clouds Media Group kwa lengo la kuwapa pole juu ya tukio la wikiendi iliyopita la RC Makonda kuingia Clouds TV akiwa askari wenye silaha za moto.

Tukio hilo limeripotiwa kwa kile kilichoelezwa kuwa RC Makonda alitaka watangazaji wa kipindi cha Shilawadu warushe kipindi ambacho hakijamalizika kwenye maandalizi yake.
A post shared by Bishop Josephat Gwajima PhD 🌍 (@bishopgwajima) on