March 24, 2017

Yafuatayo yatabadilisha maisha yako kama utayazingatia.

 YAFUATAYO YATABADILISHA MAISHA YAKO KAMA UTAYAZINGATIA/self esteem
Leo nataka kukushirikisha mambo muhimu mawili ambayo ukiyashika na kuyafuata nina uhakika na imani kubwa kuwa utakwenda kuona mabadiliko makubwa sana ya kimaisha kwako. 

Mambo haya ni muhimu uyasome kwa utulivu kisha uweze kuyafanyia kazi taratibu mpaka utakapo weza mambo haya ni kama ifuatavyo:-

1.  Chagua kilicho bora na ukifuate, 

katika maisha kuna wakati unakumbwa na ile hali ya kuwa na vitu vingi sana iwe kwa kuviona au kichwani lakini yote kwa yote nachomaanisha ni kuwa unakuwa umekumbwa na mambo mengi sana na unajikuta kuwa huwezi kufanya maamuzi, sasa njia iliyo bora na sahihi pale unapokumbwa na machagulio mengi ni kuchagua kitu kilicho bora. 

Nakushauri uchague kitu bora na sio bora kwa nani au nani bali bora kwako. Usichague kitu ukasema ni bora eti kwa kuwa umeona kuwa kuna mtu fulani kasema ni bora hapana bali chagua kitu kwa kuwa wewe kwako ndicho umeona ni bora kuliko wengine. Hili nimeliongea kutokana na sababu kuwa kuna watu wamekuwa wakipata shida sana katika kuchagua vitu kama kazi za kufanya.

Mfano utakuta mtu hachagui kazi ya kufanya kutokana na ubora wa kazi au uwezo wake juu ya kazi bali yeye anachagua kazi kutokana na ubora wa mshahara, pindi apatapo kazi hiyo ndipo hujikuta sasa akiwa ameanza kulalamika kuwa oooh sijui hii kazi vipi sijui ile kazi vile. Sasa kwanzia leo hakikisha unachagua kilicho bora kwako. Iwe shule, iwe chuo, iwe kazi, iwe biashara, iwe mahali pa kuishi n.k.

2.    Acha kuwa zima moto, 

Naposema acha kuwa zima moto narejelea ile hali ya kukosa msimamo,hali ya kukosa hamasa, hali ya kuhairisha mambo ovyo na ile hali ya kuto kutulia katika shughuli moja. Hiki ndicho nacho maanisha napo sema acha kuwa zima moto. 

Sasa ukiangalia kikosi cha zima moto chenyewe kipo maalumu kwa ajili ya uokozi wa majanga ya moto tu na sio wakati mwingine hivyo kama hakuna moto sehemu zima moto huwezi kuwaona. 

Sasa ikoje katika mafanikio, kitu kinachokuja kutokea katika mafanikio ni kuwa kuna watu wamekuwa zima moto yaani hawa ni wale ambao wakitoka kwenye semina,wakisoma vitabu au kusikiliza kanda za sauti wanatoka na hamasa kubwa na ahadi nyingi kuwa hili ntalifanyia kazi na lile pia ntalitekeleza lakini watafute baada ya siku mbili utakuta wako kule kule walikokuwa kabla ya semina au kusoma kitabu fulani. 

Kuna watu mfano huwa hawaendi hospitalini kuchunguza afya zao labda mpaka wawe wanaumwa au wamezidiwa sana, jambo ambalo sio zuri sana kwa afya zetu. Kuna watu hawawezi kufanya kitu fulani mpaka wawe wameambiwa au wametishwa na mtu fulani jambo ambalo ni hatari sana watu wa namna hii ndio nao waita kina zima moto. 

Kama nawe ni mmoja wapo basi acha mara moja, usisubili mpaka maji yamwagike ndipo uanze kujiuliza kwanini yamemwagika ili hali uliziona dalili za maji kumwagika na haukufanya lolote. Waswahili husema “usipoziba ufa hautojenga ukuta. 

Acha kuwa zima moto kwanzia sasa usisubiri yakukumbe ndipo utende.