March 11, 2017

Billionea huyu wa kitanzania avunja rekodi ya mabillionea wa Africa.

Mkurugenzi wa Mohammed Enterprises (METL), Mohammed Dewji ameifanya Tanzania kuwa moja kati ya nchi saba za Afrika zenye mabilionea.

Akiwa na miaka 41, Dewji ametajwa na gazeti la Forbes kuwa ndiye bilionea kijana zaidi kwenye orodha ya mabilionea 21 wa Afrika iliyotolewa Januari 5 mwaka huu.


Kwa mujibu wa viwango vya utafiti wa gazeti hilo, wastani wa Waafrika kuwa mabilionea ni miaka 63 lakini Dewji amefanikiwa kufika huko baada ya kuisimamia vyema kampuni hiyo iliyoanzishwa na baba yake miaka ya 1970.


Kutokana na mafaniko aliyojengewa na familia yake, Dewji ameahidi kutumia nusu ya utajiri wake kuwasaidia watu wasiojiweza kutoka taasisi mbalimbali  kukabiliana na umaskini.