May 9, 2017

Mambo muhimu ya kufanya asubuhi ili ufanikiwe.

 MAMBO MUHIMU YA KUFANYA ASUBUHI ILIUFANIKIWE
1. Fanya Sala
Mara tu uamkapo asubuhi hakikisha unafanya sala, sala ya shukrani ni muhimu sana kwasababu, hakuna kitu cha msingi unachoweza kufanya katika maisha yako kama kushukuru kwa nafasi uliyo pewa kuiona siku mpya. shukuru kwa kila nafasi unayoipata katika maisha yako. shukrani ni kitu kikubwa sana ambacho unaweza kukifanya mara tu uamkapo asubuhi.

2. Fikiria Malengo yako
Fikiria malengo yako mara kwa mara, jenga utamaduni wa kusoma mara kwa mara malengo yako ili kuweza kujikumbusha na kujua unatakiwa kufanyanini. kuna faida kubwa katika akili yako kwa kufanikisha yale unayo yataka. kumbuka kusoma mara kwa mara malengo yako.

Soma: vitu saba muhimu vitakusaidia kufikia malengo yako

3. Fanya mazoezi
Ni vema na busara ukajali afya yako kwa kufanya mzoezi, mazoezi yanafaida nyingi sana kwenye maisha ya mwanadamu, mazoezi yanajenga uimara katika akili yako na kukuongezea uwezo wa kufikiri lakini siyo hivyo tu, yanakupa uwezo wa kuvumilia kufanya kazi kwa muda mrefu hasa ukizingatia kwa nyakati za sasa ambapo unahitajika kufanya kazi masaa mengi zaidi.