May 11, 2017

Hii ndio list ya mataifa yenye watu warefu zaidi Duniani - Utafiti.

Utafiti mpya umeonesha kwamba wanaume wa Uholanzi ndio warefu zaidi duniani, na upande wa wanawake, wanawake wa Latvia ndio warefu zaidi.

Kimo cha wastani kwa wanaume Uholanzi ni futi 6 kwa sasa (sentimita 183), na kimo cha wastani kwa wanawake wa Latvia ni futi 5 inchi 7 (sentimita 170).

Utafiti huo, ambao matokeo yake yamechapishwa kwenye jarida la eLife, umefuatilia kimo cha watu na mabadiliko yaliyotokea katika mataifa 187 tangu 1914.

Mataifa yenye wanaume warefu zaidi duniani 2014 (kwenye mabano ni nafasi iliyoshikiliwa 1914):

 1. Uholanzi (12)
 2. Ubelgiji (33)
 3. Estonia (4)
 4. Latvia (13)
 5. Denmark (9)
 6. Bosnia na Herzegovina (19)
 7. Croatia (22)
 8. Serbia (30)
 9. Iceland (6)
 10. Jamhuri ya Czech (24)

Mataifa yenye wanawake warefu zaidi duniani 2014 (kwenye mabano ni nafasi iliyoshikiliwa 1914):

 1. Latvia (28)
 2. Uholanzi (38)
 3. Estonia (16)
 4. Jamhuri ya Czech (69)
 5. Serbia (93)
 6. Slovakia (26)
 7. Denmark (11)
 8. Lithuania (41)
 9. Belarus (42)
 10. Ukraine (43)