May 2, 2017

Fundisho kwa kina-dada wote wanaotaka kuolewa.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook Mwanasaikolojia Chris Mauki afunguka na kusema haya machache lakina yenye maana kubwa.


"Achana na zile ndoto na matamanio eti ya kuolewa na mwanaume mwenye kila kitu, mwenye maisha yake, unaingia unakuta usafiri upo kwa ajili yako, nyumba, mashamba, viwanja, maduka na vyanzo vingine vya pesa halafu unazuga eti ulimpenda toka moyoni kumbe umeingia kuendeleza safari ya matumaini aliyoianza mwenzako, huo ni ukupe tu, tamani kupata utakayeanza naye maisha, mchume pamoja ili upate hata chembe ya uhuru wa kusema hivi ni vyetu.
We vipi? Yani ulichoshiriki kuzalisha ni watoto tu? Ngoja nikutoe tongotongo leo ili upone, au kawaulize walioingia wakakuta kila kitukipo jinsi wanavyovumilia shida. Kawia ufike."  Chriss Mauka.