May 13, 2017

Makosa matatu ya kuepuka kenye mahusiano

 MAKOSA MATATU YA KUEPUKA KENYE MAHUSIANO
1 Kuonyesha tabia mbaya

Katika mapenzi na maisha, hakuna kile ambacho kinajalisha zaidi kuliko matendo. Kama utajiheshimu wewe mwenyewe, watu pia watakuheshimu – na wanawake watapendezwa na hili jambo na watajaribu kuleta uunganishi na wewe. 

Isikupite Hii: Athari Za Mahusiano Ya Uchumba Ya Muda Mrefu Kupita Kiasi (Miaka 2 - 4)

So usiseme maneno ambayo hunuwii kusema na usivunje ahadi zako. Jiamini kila wakati, na pia ni muhimu upate kujua vile ambavyo watu watakuchukulia kabla haujatamka jambo lolote. Kumbuka: kama utaonyesha mambo chanya kila wakati, basi kuna uhakika wa juu kwa wanawake kukuandama na kutaka kutangamana na wewe kila wakati.

2 Kuwa na confidence ya chini

Katika macho ya mwanamke, hakuna kitu ambacho kinamfurahisha na kumsisimua kama kumuona mwanaume ambaye ana confidence. So usijaribu kuonyesha watu kuwa 'unaweza' kuwafurahisha; hii inaweza kuonyesha unyonge wako. Kama wewe unajiona kama ni mfalme wa hii dunia, basi wanawake watafikiria vivyo hivyo. 

Isikupite Hii: Siri 9 Zitakazonfanya Ndoa Yenu Kuwa Na Furaha Daima.

Lakini hii haimaanishi kuwa unapaswa kuvuka mipaka ya kuonyesha confidence zako mbele ya mwanamke. Haina haja ya wewe kuonekana kama fala ama kujisifu kwa jinsi vile ulivyo mkali ikija na maswala ya kuwatongoza wanawake wa aina yoyote.

3 Kudanganya

Kudanganya kiasi kunakubalika. Lakini, kudanganya mara kwa mara kutaishusha hadhi na uaminifu wako mbele ya wanawake. Kando na hapo kudanganya sana kunaweza kukakujeukia siku moja au nyingine.

Isikupite Hii: Unapoanza Mahusiano Mapya Epuka Wanawake Wa Aina Hii.

Kwa bahati mbaya, wanaume wengi wanaamua kudanganya ili kuweza kuondoa ule wasiwasi wa kusema au kuongea ukweli. 

Lakini kile kitu ambacho unasahau ni kuwa ukidanganya, kuna siku ambayo unaweza kushikwa; na ukishikwa utakuwa umeharibu sifa zako zote ambazo ulikuwa ukijenga. So ni bora zaidi uongee ukweli na uhakika. Kama unashindwa na la kumwambia mwanamke, basi ni bora zaidi kunyamaza kuliko kudanganya.

Hii pia inaenda kwa ile tabia ya kudeti wanawake wengi wakati mmoja. Badala la kuruka deti moja hadi nyingine na kuomba kuwa hakuna mmoja atakayejua, ni bora zaidi kuwaambia kuwa hauko tayari kuingia katika jukumu lolote na yeyote. Hii itakusaidia kupunguza wasiwasi ambao ungekuwa nao.

Kama umefanya kosa lolote katika haya ambayo tumetaja, jambo ambalo unatakiwa kufanya ni kusoma kutokana na makosa haya. Baada ya muda mfupi utaona utofauti katika maisha yako ya kudeti