May 30, 2017

Mambo 5 muhimu ambayo mke huyahitaji kwa mume.

KUTATULIWA MATATIZO
Wanawake wengi hutegemea kuwa wanapokuwa na wapenzi watasaidiwa katika matatizo ya kimaisha na migogoro ya kimawazo, kwa mfano ushauri juu ya maisha yao, kulindwa na hatari za kimaisha, kusaidiwa katika shida na kuongozwa pale wanapohisi kushindwa kufanya jambo.

Soma: Mambo 15 Mwanamke Anayoyaangalia Kabla Ya Kukupenda.


KUBEMBELEZWA
Wanawake hupenda kubembelezwa pale wanapokuwa na huzuni, wengi wao hawapendi kukaripiwa, mara nyingi hupenda kuungwa mkono wanapokuwa na misuguano na wengine, ili mwanaume amteke kimapenzi mwanamke lazima awe nyuma yake hata kama atakuwa na kosa wanawake wengi hupenda  kuelimishwa zaidi kuliko kufokewa.

KUWA NAMBA MOJA
Safari ya penzi la mwanamke haishii kwenye kumpata na kumliki, kisha kujisahau kwa kisingizio kuwa umemuoa au umemvisha pete ya uchumba, ni zaidi ya hapo. Jambo la tatu ambalo wanawake wengi huhitaji ni kuwa  namba moja au kupendwa.

Wanapenda watangulizwe katika mapenzi na kusiwepo na mwingine wa kuchukua nafasi yao katika mazungumzo na mapenzi kwa ujumla. Wanawake hawapendi kuitwa majina mabaya kwa mfano mjinga, malaya au kulinganishwa na wanawake wenzao wabaya.

KURIDHISHWA KWENYE TENDO
Hata kama utakuwa na kiwango kikubwa cha mapenzi juu ya mpenzi wako kwa kiwango gani, ukiwa dhaifu katika tendo la ndoa utayumbisha penzi lako.

Ni wajibu wa mwanaume kuhakikisha kuwa anamtosheleza mpenzi wake katika tendo hilo, utundu unahitajika ili kumkata kiu mpenzi wako.

Soma: Kwanini Wanaume Wengi Walioko Kwenye Ndoa Wanakufa Mapema Na Kuwaacha Wake Zao?

MAZUNGUMZO
Wanawake wanatajwa kuzungumza maneno 25,000 kwa siku, huku wanaume wakibaki na kiwango cha maneno 5,000 kwa siku, hii ikiwa na maana kuwa wanawake hupenda zaidi kujieleza walivyo mbele ya wengine, kwa msingi huo wakizuiwa wasiongee hujiona kama wanakosa nafasi muhimu ya kueleza mawazo yao, hivyo kama una mpenzi wako mpe uhuru wa kuzungumza na kumsikiliza bila kumkatiza kwa ukali.