May 9, 2017

Hizi hapa faidia nne '4' za ndoa.

Wanawake wengi ambao hawajaolewa (Singles) wanaweza wakaangalia baadhi ya ndoa za marafiki zao na kuona mahusiano mabovu na wanandoa ambao hawana raha, lakini sio tu kwasababu eti baadhi ya wapenzi siku hizi hawaipi ndoa kipaumbele, haimaanishi kwamba ni bora zaidi kuishi kivyakovyako maisha (Stay single for life), anasema Rabbi Shmuley, anapozungumzia faida za ndoa.

Soma: Hizi Ndizo Sifa Za Mume Bora 'husband Material'.

Rabbi Smuley, ambaye ni mtaalamu wa masuala ya kijamii, kwa mfano; ndoa, mahusiano, malezi ya watoto, na pia muandishi wa vitabu 18 vyenye mauzo ya juu (Best-Selling author); anatupa faida 4 za kuwa ndani ya ndoa:

1. Utulivu na mshikamano wa watoto. 
Rabbi Shmuley anasema kwamba watoto wananufaika sana wanapolelewa katika nyumba ya wazazi wawili, yaani baba na mama.

2. Una mtu wa kushirikiana nae kimaisha. 
Kutoka kujenga familia mpaka kushirikiana majukumu na masuala yanayohusiana na majukumu hayo. Rabbi Shmuley anasema ndoa inatoa faida nyingi za muda mrefu katika masuala haya.

3. Maisha marefu. 
Rabbi Shmuley anasema baadhi ya tafiti zimeonysha kwamba wanandoa wanaishi maisha marefu na wana raha kuliko wale wasio kwenye ndoa.

Soma: Sifa 7 Za Mwanamke Wa Kuoa (Wife Material).

4. Suala la kujamiina. 
Wanandoa wana ushirika wa uhakika linapokuja suala la kujamiina, na Rabbi Shmuley anasema hili lina faida kwa mwili na akili (mind and Body) vitu ambavyo ni muhimu kwa maisha ya mwanaadamu.