May 23, 2017

Nguvu ya maamuzi katika kuyafikia maono( PART 2)

Nguvu ya maamuzi ni nguvu ya kuwa ili ufanikiwe  kwenye  maisha ni lazima ufanye maamuzi leo kwa jicho la kesho Mr. Yopace

Ili kuwa na Maamuzi bora  yatakayoleta  mafanikio ni lazima uwe na: maono, ndoto na malengo; ni lazima ujue wewe ni nani? upo duniani kwa ajili gani? unataka kuwa nani? na unataka kufanya nini? Maandiko yamenena wazi “pasipo maono watu huacha kujizuia” maono yanakusaidia kujua wapi unatakiwa kwenda, nini unatakiwa kufanya na nini  hupaswi kufanya. 

Maamuzi bora ni yale ambayo yanakufanya ufikie maono na ndoto  ulizo nazo, ama ni maamuzi ambayo hayaleti uharibifu wa hatima yako. Yapo maamuzi ambayo huweza kuonekana kuwa ni mazuri kumbe hutupelekea katika uharibifu - Mithali 14:12.


Maamuzi ni jambo la kimwendelezo unachokiamua leo kina uhusiano mkubwa sana na kitakachotokea kesho. Maamuzi  yanaweza yakakufanya ufikie maono yako ama yakaharibu maono na ndoto ulizo nazo. Maamuzi bora ni maamuzi yanayofanywa kwa kuyatazama maono na ndoto ulizo nazo.  Maono na ndoto vifanyike sababu ya kila maamuzi unayoyafanya, usifanye jambo lolote leo lenye madhara kesho haijalishi jambo hilo linauzuri kiasi gani kwa sasa  kwa sababu.
Gharama ya kuyazuia madhara kesho yaliyosababisha na maamuzi ya leo ni kubwa sana kuliko kuzuia manufaa ya leo yenye madhara kesho - Mr. Yopace
Ili kuyafikia maono na ndoto tulizonazo ni lazima tukubali kuingia gharama ya kuwa waaminifu katika kulinda maono tuliyonayo... 
INAENDELEA................