May 18, 2017

Nguvu ya Maamuzi (PART 1)



Maisha ni matokeo ya maamuzi; umefanikiwa ama haujafanikiwa, tajiri ama maskini, mwenye tabia mbaya ama nzuri.

Kinachotofautisha mtu na mtu ni tofauti ya maamuzi. Unaamua uwe mtu wa aina gani, uishi maisha gani, vile ulivyo leo ni matokeo ya maamuzi ulioyafanya kabla ya leo, kama huipendi leo yako badilisha maamuzi yako ili leo yako isifanane na kesho yako. Huwezi kuibadilisha leo yako ila kesho yako. Jana yako ndiyo iliyokusababishia leo yako.


Uzuri au ubaya wa maamuzi ya leo hupimwa na matokeo ya kesho Maamuzi mabaya huleta kesho mbaya Maamuzi mazuri huleta kesho nzuri - MR. YOPACE


Maamuzi ni pale unapochagua jambo moja kati ya mambo mengi,  unapochagua kwenda njia moja kati ya njia nyingi, maamuzi yamebeba hatima ya maisha, maamuzi hutengeneza mfumo wa maisha ya mtu, maamuzi ni kukubali kuingia gharama; Kuna wakati maamuzi yanakutaka uchague jambo moja tu na uachane na mengine yote kuna wakati pia maamuzi yanakutaka uweke vipaombele jambo lipi lianze na lipi lifuate. 

Kila maamuzi yana matokeo ambayo huweza kuwa mazuri ama mabaya Wapo watu wanaofurahia matokeo ya maamuzi yao vile vile wapo wanaojutia matokeo ya maamuzi yao.
           

Jana yako hukufanya maamuzi sahii ndio imesababisha leo yako iliyojawa shida, uchungu na majeraha ya nafsi. Kumbuka kwamba unaweza  kuibadilisha kesho yako kwa kubadilisha maamuzi leo;  unataka kesho yenye furaha yenye baraka yenye mafanikio fanya maamuzi sasa yatakayo badilisha mfumo wako wa maisha. 

Usiitazame tena jana yako tazama kesho yako amini katika kesho yako hali yako ya sasa isikukatishe tamaa  vaa ujasiri, kuwa makini na maamuzi ya sasa ili yakuletee kesho unayoitarajia.


Maamuzi ni jambo la kimfumo ubora wa maamuzi ya mtu hutokana na namna mfumo wake wa fikra ulivyoathirika.  njia pekee ya kufanya maamuzi yako kuwa mema ni kuathiri mfumo wako wa fikra kwa mambo mema - MR. YOPACE  
Mtu mwema katika akiba njema hutoa mema  na mtu mbaya katia akiba mbaya hutoa mabaya” Inaendelea.........

Emmanuel Mwakyembe (MR. YOPACE) +255716531353