May 28, 2017

Nguvu ya maamuzi part 3 Kiini cha maamuziKINACHOMFANYA MTU ATOE MAAMUZI MABAYA AMA MAZURI NI MAMBO YALIOUJAZA MOYO WAKE KINACHOUJAZA MOYO NA NAFSI YA MTU HUMTENGENENEZEA MTU HUYO NAMNA YA KUONA (IMANI) NA NAMNA YA KUYACHUKULIA MAMBO (MTAZAMO) 
   MR YOPACE                  
 (Mathayo 12:35) “Mtu mwema katika akiba yake njema hutoa mema  na mtu   mbaya katika akiba mbaya hutoa  mabaya”
(Mithali 23:7)  “Maana aonavyo nafsini mwake ndivyo alivyo”

kitabu cha Mithali 4:23 Ukisoma kwa tafsiri ya kingereza“Be careful the way you think your life is shaped by your thought”
Maana yake kuwa makini na namna unavyofikiri ,maisha yako ni matokeo ya fikra zako

Vile vitu ambavyo mtu huambatana navyo ndivyo vitu ambavyo vinapata nafasi kubwa ya kuathiri nafsi yake au kuujaza moyo wake, Kwa mfano;aina ya vitabu anavyosoma, aina ya mziki anaopendelea kusikiliza, aina ya marafiki alionao. aina ya program za televishion anazopendelea kuangalia, aina ya mambo anayopenda kuyaperuzi kwenye mitandaoya kijamii Na kwenye intanet. Pia hapa hujumuisha mambo yote ambayo mtu huyu hupendelea zaidi kuyaona kuyasikia na kuambatana nayo kwa muda mwingi
Vitu hivi ambavyo mtu huyu huambatana navyo humtengenezea mambo makubwa mawili :
-{namna ya kuamini –beliving system}
-{namna  ya kuyachukulia mambo-mtazamo(altitude)
Namna ya kuamini + namna kuyachukulia mambo= Aina ya maamuzi

“Namna ya kuamini na mtazamo wa mtu,  ni kama sumaku kwenye moyo wa mtu ambayo huvutia zaidi na kutoa nafasi kubwa zaidi kwa mawazo ambayo hayakizani na vitu ambavyo mtu huyu hupendelea zaidi kuambatana navyo , kwa sababu Maamuzi ya mtu hutegemea wazo lililopata nafasi zaidi kwenye moyo au fahamu za mtu hivyo, maamuzi ya mtu huyu yatafanana na vitu anavyoambatana navyo” MR. YOPACE

 Aina ya maamuzi ambayo mtu huyafanya kwa kujirudia rudia yanapata nafasi zaidi kwenye moyo wa mtu humtengenezea mtu huyo Tabia na tabia hiyo inapojirudia mara nyingi zaidi hutengeneza Mazoea (addiction)
 HIVYO MTU AKITAKA KUBADILISHA AINA YAKE YA MAAMUZI AU AACHANE NA TABIA FULANI ZISIZOFAA NI LAZIMA ASHUGHULIKIE KWANZA KIINI CHA TATIZO AMBACHO NI VITU ANAVYOAMBATANA NAVYO
 Kila kitu ambacho mtu anaambatana nacho ni lazima kiwe kinamchango fulani chanya kwenye maisha.

Msingi mzuri wa kuzingatia unapochagua vitu au watu wa kuambatana nao
 -WAWE NI WATU AU VITU VINAVYOKUPA FURAHA NA AMANI
-WATU AU VITU AMBAVYO HAVIHARIBU UHUSIANO WAKO NA MUNGU
-WAWE NI WATU AMA VITU VINAVYOKUPA CHANGAMOTO CHANYA  ZA KIMAENDELEO
-WAWE NI WATU AU VITU VINAVYOKUSOGEZA KWENYE --MAONO YAKO, NDOTO ZAKO NA KUKUFANYA UISHI SAWA SAWA NA KUSUDI ULILOITIWA

  Ukitaka kubadilisha  aina ya maamuzi yako,tabia yako,aidha ukitaka kutengeneza kesho yako njema utakayoifuraia ni lazima uamue  kufanya maamuzi magumu ya kuacha kuambatana na kitu chochote ama mtu yeyote Yule ambaye hana tija kwenye maisha yako, kwa sababu vitu unavyoambatana navyo ndivyo vinavyoujaza moyo wako na ndivyo vinavyopelekea mtazamo wako na namna ya kuamini kwako  ambavyo ndivyo msingi wa maamuzi yako ambavyo pia hukutengenezea tabia.
Ni lazima ufike mahali ujiulize kuhusiana na marafiki unaoambatana nao, vitabu unavyovisoma, aina ya mziki anaopendelea kusikiliza, aina ya program za televishion anazopendelea kuangalia, aina ya mambo unayopenda kuyaperuzi kwenye mitandaoya kijamii Na kwenye intaneti ,aina ya burudani unazopendelea, Je vina tija kwa maisha yako
Mafanikio ya mtu huanzia kwenya uchaguzi  uchaguzi mbaya hupelekea uangamivu  na uchaguzi mzuri hupelekea mafanikio
                   INAENDELEA……………………..
EMMANUEL MWAKYEMBE (MR. YOPACE)
Mobile: +255716531353
Email: emamwakyembe@gmail.com