May 11, 2017

Je, ni sawa kwa wanandoa kupokea simu ya mume/mke?

Hii inatokea sana katika ndoa mume au mke kupokea simu isiyokuwa yake na mara nyingi hupelekea ugomvi mkubwa kwa wanandoa, unaweza kujiuliza maswali mengi sana ambayo ukakosa majibu yake kuhusiana na hili. 

Wakati mwingine mmoja kati ya mke au mume anaweza kuwa tayari kupokelewa simu zake wakati mwenzake hayupo tayari hivyo ni changamoto. 

kwa majibu ya harakaharaka unaweza sema inawezekana kukawa hakuna uaminifu kati ya hawa watu wawili sababu kama ni dhahili inajulikana fulani mke wa fulani au fulani mume wa fulani, basi mke na mume awe huru kuwa wazi hata katika hili, Kutokana na muda mrefu wawili hawa wameishi pamoja inafika kipindi marafiki wa mume wanakuwa wa mke na marafiki wa mke wanakuwa wa mume, sasa kuna haja gani ya kuwekeana mipaka katika simu. 

Mara nyingi simu huleta ugomvi mkubwa sana sio tu kwa wanandoa hata katika mahusiano ya kila siku, Matumizi ya simu yamekuwa makubwa kiasi ambacho yanaathiri mawasiliano ya ana kwa ana ya watu. 

Kuna familia ambazo kila mtu akiwa na simu yake basi hakuna tena ile desturi ya watu kukaa pamoja kuongelea mambo mbalimbali kuhusiana na familia, kila mtu anjifungia chumbani bize na simu yake kuperuzi mitandao ya kijamii wakati mwingine hata waliopo ndani ya familia hutumia simu kuwasiliana wakiwa ndani ya nyumba. 

Je nini maoni yako kuhusiana na mke au mume kupokeleana simu?