Featured Posts

May 2, 2017

Siri unayotakiwa kuijua wewe mke au mume.

 SIRI UNAYOTAKIWA KUIJUA WEWE MKE AU MUME
Yako mambo ambayo ni muhimu kukumbuka katika suala zima la kutoa na kupokea baina ya mume na mke katika ndoa. Mwanaume anapoonyesha kutaka au kuhitaji kitu kutoka kwa mwanamke, mwanamke huhamaki, wakati mwanaume akitoa kitu kumpa mwanamke, mwanamke huitika kwa hujisogeza karibu na mwanaume (hapa namaanisha kuwa mwanamke anapopokea kitu kutoka kwa mwanaume yeye hujikuta anaongeza kuwa karibu zaidi na mwanaume huyu kuliko wakati ambao mwanamke ndiye anayempa kitu mwanaume). 

Soma: Je Unaijua Saikolijia Ya Mwenzi Wako Katika Mahusiano

Katika asili hii utaona uhalisi wa mwanaume kumtimizia mahitaji mwanamke na sio mwanamke kumtimizia au kumtunza mwanaume (ni jambo la asili mwanaume kumpa mahitaji mwanamke na sio mwanamke kumpa mahitaji mwanaume). Mwanaume anapojitoa kwa moyo kwa ajili ya mwanamke, mwanamke kunyenyekea bila shuruti. 

Hakuna kilicho cha thamani sana kwa mwanamke zaidi ya mwanaume mwenye uwezo wa kujitoa kwa moyo wa dhati kwa ajili ya mke wake. Hakuna kinacho muumiza na kumkatisha tamaa mwanamke kama kuwa na mwanaume asiyeweza kujitoa kwa moyo wa dhati kwa ajili ya mke wake. 

Ngoja nikushirikishe siri iliyopo hapa; Kama unatamani kuwa na mwanamke mnyenyekevu basi jifunze kujitoa kwa moyo wa dhati kwake, unapoonyesha kutaka kumuumiza mkeo, mkeo naye kuonyesha kujihami au kukukwepa. 

Pale mwanaume anapomshirikisha mwanamke na mwanamke naye huongeza kumjali mwanaume. Mwanaume anapoonyesha kuongoza, kwa uongozi wenye uwajibikaji, basi na mwanamke naye huonyesha kufuata uongozi ule. 

Uongozi hapa simaanishi kuwa bosi wa mkeo, kila siku unatoa amri za nini unataka kifanywe na kifanywe vipi, la hasha, kwa kuwa kiongozi hapa namaanisha kutangulia mbele na kuwaonyesha wengine njia, sio wewe kuwaweka wengine mbele wakati wewe unakwepa au unahofia hatari. 

Soma: Mambo 15 Mwanamke Anayoyaangalia Kabla Ya Kukupenda


Kuongoza hapa namaanisha kumwonyesha mwenza wako namna bora ya kufanya au namna bora ya kuenenda. Ukisema hutaki kitu fulani basi unaonyesha kwa vitendo nini unachokitaka na kwanamna gani unakitaka kiwe au kifanywe.