May 17, 2017

Utajengaje tabia bora na za kudumu katika mafanikio yako?

 UTAJENGAJE TABIA BORA NA ZA KUDUMU KATIKA MAFANIKIO YAKO!!
Msingi mkubwa wa mafanikio yoyote yale unajengwa na tabia. Hiyo ikiwa na maana kwamba tabia ndizo zinatusaida kujenga mafanikio ya aina fulani.

Isikupite Hii: Njia Kuu Nne Za Kuweka Akiba

Hivyo kwa mantiki hiyo, ni muhimu kujenga tabia bora za kudumu ili kuweza kufanikiwa. Je, tunawezaje kujenga tabia bora za kudumu?

1. Jiwekee malengo.

Ili  kufanikiwa kujijengea tabia ya kudumu unayoitaka, ni muhimu sana kujiwekea malengo ya tabia hiyo unayoitaka. Ni lazima ujue kipi ufanye na kipi usifanye ili kujihakikishia kwamba utamudu kuijenga  tabia hiyo.

Isikupite Hii: Zijue Mbinu Za Kubadilisha Maisha Yako Na Kufanya Yawe Mazuri Na Yenye Mafanikio.

Kwa mfano, kama unataka kuwa msomaji mzuri wa vitabu, ni muhimu kujijengea utaratibu wa kusoma kila siku hata kama ni kurasa mbili. Chochote  unachotaka kiwe katika tabia yako ya kudumu, kiwekee malengo.

2. Tafuta msaada zaidi.

Badala ya kukata tamaa ni muhimu kutafuta msaada kwa wale ambao wamefanikisha tabia kama hiyo unayoitafuta. Acha kujishaua sana, waulize siri ya mafanikio yao.

Isikupite Hii: Fahamu Njia Za Kupata Marafiki Na Kudumisha Urafiki

Watu hawa ambao utajifunza tabia mpya unayotaka kuijenga watakusaidia kukuweka kwenye mstari wa kufanikiwwa. Na watu hawa wanaweza wakawa ni marafiki au jamaa zako za karibu sana.

3. Badili tabia zako hatua kwa hatua.

Kama tabia unazotaka kuzibadili ni nyingi na unahamasa kubwa ya kujenga tabia ya kudumu, badili tabia hizo hatua kwa hatua. Acha kutaka kubadili tabia hizo mara moja, utakwama.

Isikupite Hii: Ili Ufanikiwe, Usiombe Ruhusa Bali Uombe Msamaha 

Kama ni unataka kusoma kitabu, acha kusoma kurasa nyingi sana kwa siku moja. Kama ni kufanya mazoezi, acha kufanya mazoezi hayo kwa nguvu sana siku moja. Jifunze kubadili kila kitu hatua kwa hatua na utafanikiwa.

4. Ondoa mawazo hasi.

Wakati upo kwenye harakati za kubadili tabia zako, amini utaweza kumudu kufanikiwa. Ondoa mawazo na kila mazingira ambayo yatakufanya ufikiri kwamba huwezi kubadilika.

Isikupite Hii: Mambo 8 Yatakayo-kufanya Uwe Na Fikra Chanya.

Kila kitu kinawezekna kwako ikiwa utakuwa chanya. Chukua hatua kila siku chanya, zinazoendana na kile unachokitaka. Kwa kufanya hivyo, utafanikiwa kufikia uwezo wako wa kubadilisha tabia hiyo

5. Tambua vizuizi.

Ni muhimu pia kutambua vizuizi ambavyo vinaweza kukuzuia wakati unabadili tabia zako. Ukishajua vizuizi hivyo inakuwa ni rahisi kuvuka na kuweza kufanikiwa.

Isikupite Hii: Hatua Tano Za Uhakika Za Kutatua Tatizo Lolote Unalokutana Nalo

Tambua kwamba bila kujua vizuizi hivyo, utashidwa kujenga tabia ya kudumu. Hiyo inakuwa hivyo ni kwa sababu utakuwa unashindwa kujua ni njia ipi sahihi utumie ili kukabiliana na vizuizi hivyo. 


6. Chukua hatua kila siku.

Kama nia yako ni kujenga tabia ya kuimba, imba kila siku. Kama nia yako ni kujenga tabia ya kuweka akiba, weka akiba hiyo kila unapopata pesa. Chukua hatua za kila tabia unayoitaka kila wakati.

Isikupite Hii: Muda Ni Sasa.! Usiogope Kuanza, Wala Usiogope Kukosea.

Kwa kadri utakavyozidi kuchukua hatua kila siku, utajenga misuri mikubwa itakayoweza kukusaidia hatimaye kuweza kufanikiwa kutengeneza tabia yako mpya  unayoihitaji.  

7. Tafuta namna ya kujipa zawadi. 

Pia unaweza ukajijengea mikakati ya kujipa zawadi fulani ikiwa utafanikiwa kujenga tabia ya kudumu. Hii ni mbinu ya kisaikolojia ambayo unakuwa kama unaidanganya akili yako ili ikisaidie kutengeza tabia unayoitaka.

Isikupite Hii: Sababu Za Kujipongeza Mwenyewe Kama Unafanya Haya

kwa kuhitimisha, hayo ndiyo mambo ya msingi yanaweza kukusaidia kuweza kujenga tabia ya kudumu katika maisha yako.