May 13, 2017

Dada utadumu kwenye ndoa yako, ukiwa na vigezo hizi 8.

kama yanavyosemwa na watu ni sanaa kama sanaa zingine zilivyo. Kama ni mchezo, basi una sheria zake. Leo saikolojia.com inakupa vigezo muhimu ambavyo, ukivizingatia, mumeo hakuachi hata kwa dawa!

Isikupite Hii: Upendo Timilifu Kwa Wanandoa Huwa Na Sifa Hizi 3.

  1. Upendo
Kila mwanaume anataka kujisikia anapendwa. Anataka kuona kuwa mwenza wake anampenda kiuhalisia na anamjali.

2. Heshima
Hata pale anapokuwa hayupo, anataka mwenzake wake awe nyuma yake, kumuongelea na kumheshimu.

3. Mapenzi

Kila mwanaume anahitaji mahaba, hapa nasema mahaba badala ya ngono, kwa sababu si kila mwanaume ni mzuri katika hilo. Mahaba ninayoyaongelea ni kupapaswa, kubusiwa au kukumbatiwa.

4. Kukubalika

Kila mwanaume anataka kujisikia mwenza wake anamkubali na kumthamini kwa mambo mbalimbali kama vile penzi lake, muda, jitihada, anavyojituma na kila anachokifanya kwa mwenza wake.

5. Yeye ni bora zaidi

Anataka mwenza wake kujisikia kuwa yeye ni bora zaidi. Kila mwanaume anataka ajisikie kuwa yeye ni mwanaume bora zaidi kuliko wote aliowahi kuwa nao, na wengine wanataka kujisikia kuwa ni mwanaume pekee ambaye umewahi kuwa naye hata kama anajua si kweli.

6. Uaminifu

Mwanaume anahitaji mwenza wake awe mwaminifu. Uaminifu husaidia kujenga mapenzi zaidi, kila kitu kwa mwanaume na kadiri mwenzake anavyokuwa mwaminifu, ndivyo hawezi kuwa na wivu kwani anakuwa ameshajiaminisha.
  
Isikupite Hii: Je Wajua!! Afya Bora Na Mpenzi Bora Huchochea Furaha Ya Maisha

7. Ukweli
Kila mwanaume anahitaji kujua kuwa anaweza kumwamini mwenza wake na kwamba naye anamwamini, ukiwa mkweli ni rahisi mume kukujengea imani, kuwa mkweli kwa kila jambo.