June 12, 2017

Hivyo ndivyo mitume wa Kristo walivyouawa. (Mashujaa wa Imani)

Mtume peke ambaye kifo chake kimeandikwa katika Bibilia ni Yakobo (Matendo Ya Mitume 12:2). Mfalme Herode alimweka Yakobo “afe kwa upanga.” Kuna uwezekano kuwa alikatwa kichwa. 

Hali ya kifo cha mitume wengine zimehusiana kutakona na vitabu vya hostoria ya Kanisa, kwa hivyo tusiweke uzito mwingi kwa tukio lo lote. 

Mtume Petero alisulubiwa kichwa chake kikiangalia chini kwa msalaba wa umbo la X huko Rumi kwa kutimiza unabii wa Yesu (Yohana 21:18). 

Mathayo aliteseka kwa ajili ya injili huko Uhabeshi, aliuwawa na donda la upanga". Yohana alikumbana na mateso juu ya injili na alichemshwa katika pipa kubwa la mfuta, wakati wa uvumi wa mateso huko Rumi. 

Ingawa aliokolewa kimuujiza kutoka kwa kifo. Yohana alihukumiwa vidimbwi vya kisinga cha Patmosi. Alikiandika kitubu chake cha unabii cha Ufunuo huko Patmosi.

Mtume Yohana baadaye alifunguliwa na akarudishwa nchi hii leo yaitwa Uturuki. Alikufa akiwa mzee, Mtume pekee aliyekufa kifo cha kawaida.

Yakobo, nduguye Yesu (si mtume halisi), alikuwa kiongozi wa Kanisa huko Yerusalemu. Alitupwa kutoka mnara wa juu sana wa Kusini-Mashariki wa Hekalu (takribani futi mia moja kwenda chini) wakati alikataa kumkana Babaye katika Kristo. Walipogundua kwamba ameponea baada ya kutupwa, walimpiga Yakobo kwa rungu hadi akafa. Hii imetuhumiwa kuwa mnara ambao Shetani alikuwa amempeleka Yesu wakati wa majaribu.

Bartholomayo, ambaye anaitwa Nathanaeli, alikuwa mmisionari huko Asia. Alishuhudia Kristo katika maeneo ya Uturuki na akauwawa ka sababu ya kuhubiri injili huko Armenia, kwa kupigwa hadi kifo kwa mjaredi.

Andrea alisulubiwa kwa msalaba wa umbo la X huko Ugiriki. Baada ya kuchapwa kwa mijaredi mingi na walinzi saba, kisha wakamweka katika msalaba ili kurefusha maumivu na machungu yake. 

Wafuasi wake wakaripoti kuwa wakati aliongozwa kuelekea kwa msalabani, Andrea akawapungukia mkono kwa maneno yafuatayo, “kwa muda mrefu nimengoja na kutamani saa kama hii ya furaha. Mslaba umekwisha takaswa kwa mwili wa Kristo ulioangikikwa juu yake.” 

Aliendelea kuwahubiria watesi wake kwa siku mbili hadi wakati alikufa. Mtume Tomaso alichomwa mkuki huko India katika safari zake kama mmisionari wa makanisa ya huko India. 

Thadayo, mtume aliyechaguliwa kuchukua nafasi ya Yuda Iskariote, alipigwa mawe na kichwa chake kutaktwa. 

Mtume Paulo aliteswa na baadaye kichwa chake kikakatwa na mfalme mwovu Niro huko Rumi katika mwaka wa A.D 67. 

Source: https://www.gotquestions.org