Featured Posts

June 6, 2017

Nguvu ya maamuzi PART 4 madhara ya maamuzi mabaya.

1. MAAMUZI MABAYA HULETA UCHUNGU NA MAJUTO 
Samson alipoamua kwenda kinyume na agizo la Mungu akampa Delila siri ya nguvu zake; alitobolewa macho na kufungwa gerezani, aliishi maisha yaliyojawa uchungu na majuto, akijutia maamuzi aliyoyafanya.Samsoni alilia kwa uchungu akimsihi Mungu.
“Ebwana Mungu unikumbuke  nakuomba  ukanitie nguvu mara hii tu  ili nipate kujilipizia kisasi kwa  kwa wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili” Waamuzi 16:28
Samsoni alikuwa na muda wa kutosha wa kujilipizia kisasi kwa wafilisti lakini maamuzi mabaya aliyoyafanya yalimfanya atamani walau dakika chache za kujilipizia kisasi 

Mara nyingi nimwesikia watu wakiongea kauli zilizoambatana na majuto na uchungu wakilaumu maamuzi waliyoyafanya katika nyakati Fulani Fulani, na kutamani muda urudi nyuma ili wafanye maamuzi upya.

Utamsikia mtu akisema "kama muda ungekuwa unarudi nyuma na mtu anapewa nafasi ya kufanya maamuzi upya basi nisingekubali kuolewa na mtu huyu au nisingekubali kumuoa mtu huyu."


Siku moja nilikuwa naongea na mzee mmoja akaniambia vile anavyojuta kwa sababu hakufanya maamuzi mazuri ya matumizi ya pesa alizokuwanazo pindi akiwa kijana aliongea kwa uchungu akisema "Nilikuwa na pesa nyingi sana sikupaswa kuishi maisha ya tabu sasa, lakini ujinga wangu uliniponza kwani pesa zote ziliishia kwenye pombe na wanawake"


Wengine husema:- 
- Najuta kwa nini sikusoma shule
- Ningejua ningetumia  muda mwingi kukaa na watoto wangu walipokuwa wadogo.
- Najuta kwa nini sikumtendea wema mke wangu mpaka akaamua  kuniacha.               
- Najuta kwa nini sikutumia ile pesa kufungua biashara.


Kila maamuzi mtu anayofanya yana matokeo ambayo mfanya maamuzi anawajibika na matokeo hayo, yawe ni mazuri ama mabaya.


2. MAAMUZI MABAYA HUKUTOA NJE YA KUSUDI LA MUNGU NA KUFUNGUA MLANGO WA LAANA.

Adamu na eva walipofanya maamuzi ya kula tunda walilokatazwa wasile, walitolewa nje ya uwepo wa Mungu na Mungu akawalaani. Mfumo wao wa maisha ukabadilika, kula kwa jasho, kuzaa kwa uchungu mauti ikaachiliwa.
Maamuzi mabaya huweza kukutoa nje ya kusudi la Mungu, nje ya maono na kukusababishia maisha ya kutangatanga, maamuzi mabaya pia huweza kusababisha laana kwenye maisha yako gharama ya matokeo ya maamuzimabaya nje ya agizo la Mungu ni kubwa sana maamuzi mema ni yale ambayo hayaendi kinyume na  agizo la Mungu
 MAAMUZI MABAYA HUSABABISHA MADHARA KWA VIZAZI VINAVYOKUJA BAADA YAKO






Maamuzi waliyoyafanya Adamu na Eva yameathili vizazi na vizazi mpaka pale Mungu alipoingia gharama kubwa ya kumnusuru Mwanadamu.

"Baba zetu walitenda dhambi  hata hawako  na sisi tumeyachukua maovu yao - Maombolezo 5:7" 

"kwa kuwa mimi Mungu wako  ni Mungu mwenye wivu  nawapatiliza wana maovu ya baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao. - Kutoka 20:5"  

Maamuzi ni jambo la kipekee sana kwa sababu matokeo ya maamuzi tunayoyafanya sisi hayatatuathili sisi tu yataenda na kwa wajukuu na vitukuu pia, na ndio maana hutakiwi tu kufanya maamuzi kwa kumfurahisha mtu Fulani kwa sababu kama leo utafanya maamuzi mabaya watoto wako na wajukuu wako wataingia katika kulipa gharama ya maamuzi uliyoyafanya.


INAENDELEA……………………………….

Emmanuel Mwakyembe (Mr. Yopace) 
Mobile: +255716531353
Email: emamwakyembe@gmail.com