Featured Posts

June 15, 2017

Nguvu Ya Maamuzi Part 5 Mungu au Mali na Pesa?


Pesa na mali ni kati ya vitu vyenye nguvu kubwa ya kuchochea maamuzi ya mtu  kwa sababu pesa hutoa majibu ya changamoto nyingi zinazoyakabili maisha ya mwanadamu, tunatumia pesa kujipatia mkate wetu wa kila siku, kuyafanya maisha yetu kuwa bora,tunafanya kazi ili tupate pesa nguvu kubwa  na muda mwingi kwenye maisha ya mwanadamu hutumika kwa ajili ya kutupa uhakika wa kipato 

Pesa na mali ndiyo huweka matabaka kati ya mtu na mtu, ama kati ya kundi Fulani la watu na kundi jingine. Pesa na mali ndiyo imefanya wengine kuwatumia wengine na pia wengine kuwatumikia wengine ,pesa na mali vimewapatia wengine heshima na kufanya wengine wadharaulike pesa na mali shetani huvitumia kuchochea maovu na kushawishi watu kufanya maamuzi potofu
wapo wanaotumia pesa kudanganya wengine, pesa imetumika kunyanyasa wengine na kudhulumu haki ya wengine,pesa imetumika pia kudharirisha utu wa wengine  na pesa imewafanya pia wengine kuishi maisha ya starehe na anasa na pia pesa imewafanye wengine waishi maisha ya utumwa,
pesa inanguvu kubwa sana ya kuchochea Maamuzi ya mtu Maandiko yanatuonya hatari ya pesa na mali jinsi ambavyo  vina nguvu kubwa ya kushawishi maamuzi yetu 

maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na imani na kujichoma kwa maumivu mengi 1 Timotheo 6:10

Kupenda pesa ni shina, ni chanzo,ama ni kichocheo cha mambaya,uovu na uasi
Lugha iliyotumika hapa ya Kupenda pesa maana yake ni kuitumikia pesa ama ni pesa kuwa na amri kwenye maamuzi yako ama kupenda pesa ni pale ambapo “maamuzi yako yote kuhusu maisha yamewekwa chini ya utii wa Nguvu ya pesa na mali
Amri ya kwanza iliyokuu “mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote” mathayo22:37
Anaposema mpende Bwana Mungu wako maana yake ni kumpa Mungu nafasi ya kwanza na kutii amri yake pia tunaweza kusema ni Mungu kuyatawala maisha yako na kuongoza maisha yako
Hatari ya pesa na mali ni kwamba vinaweza kabisa kuchukua nafasi ya Mungu Kwenye  Moyo wa mtu “Kama mtu anaweza kumpenda Mungu kwa moyo wake wote na kwa roho yake yote na kwa akili zake zote kwa maana ya kwamba maamuzi yake yote kuhusu maisha yamewekwa chini ya utii wa agizo la Mungu Vivyo hivyo ujue wazi kabisa kuwa Mtu anaweza kuipenda pesa kwa moyo wake wote kwa roho yake yote na kwa akili yake yote kwa maana ya kwamba maamuzi yake yote kuhusu maisha yakawa chini ya utii wa Nguvu ya pesa na mali          
“Bali utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake na mengine yote mtazidishiwa”
Fahamu zetu na nafsi zetu  zinatakiwa vimuelekee Mungu kwanza na sio mali wala pesa tulizonazo. Mungu anatakiwa apewe nafasi ya kwanza kwenye mioyo yetu na sio Mali   Mungu alipokuwa akitafuta nafasi ya kwanza kwa Ibrahimu alimwambia ibrahimu  mtoe Isaka sadaka,  Ibrahimu hakujali kuwa isaka ndiye mtoto pekee aliyenaye  aliruhusu moyo wake kujiachilia kwa Mungu na kumuamini Mungu
Tajiri mmoja alimfuata yesu na kuuliza afanye nini ili aurithi ufalme wa Mungu Yesu  akamwambia auze kila alicho nacho  awape masikini ndipo amfuate  Yule tajiri alihuzunika kwa sababu alikuwa  na mali nyingi ndipo yesu akasema itakuwa ni vigumu sana kwa wenye kutegemea mali kuingia katika ufalme wa Mungu  Marko 10:17-25
 Mali na pesa zikichukua  nafasi ya kwanza kwenye moyo wako ndizo zitapelekea maamuzi yako yote   Vivyo hivyo Mungu akiwa na nafasi ya kwanza kwenye Moyo wako atatawala maamuzi yako yote .
Haijalishi una mali kiasi gani Mungu amekupa kwa ajili yake  Mwenyewe  yaani kwa ajili ya utukufu wake
Maandiko yanasema muheshimu Mungu kwa mali yako na kwa malimbuko ya mazao yako
Unapochagua  kupenda pesa na mali na kuvipa nafasi ya kwanza ndani ya moyo wako gharama yake ni Kuipoteza Nafsi yako yenye thamani
“ itakusaidia nini kuupata ulimwengu Wote na kuipoteza nafsi yako yenye thamani
Ikabidhi nafsi yako kwa Mungu yeye achukue usukani kwenye uongozi wa maamuzi yako yote kuhusu pesa na mali  Baraka zako na mafanikio yako yatokane pia yaratibiwe na  na yeye  na hii ndio njia pekee ya  ya kuiponya nafsi yako Kama maandiko yanavyosema wazi kwamba Baraka za Mungu haziambatani na  huzuni kwazo
INAENDELEA......................
Emmanuel Mwakyembe
+255716531353
emamwakyembe@gmail.com