July 25, 2017

Ijue nguvu ya zawadi kwenye mahusiano.

 IJUE NGUVU YA ZAWADI KWENYE MAHUSIANO

1. ZAWADI ZINABORESHA MAHUSIANO: 

Umuhimu wakwanza wa Zawadi katika mapenzi ni kuboresha mahusiano. Fahamu kuwa unapompa mpenzi wako zawadi utamfanya ajihisi kama niwapekee kwako hivyo atajiona kama ni mmoja wapo kati ya watu wenye thamani kwako na ataamini kama kweli upo karibu yake na unamjali hivyo hatashindwa kulipa mazuri kwako kwa kukuonesha upendo wa dhati na utamfanya azidishe mapenzi kwako kwani atakua anajua kuwa wewe unamjali na unamuonesha upendo sasa kwanini nayeye asikujali?! Hivyo zawadi yako itakuwa ni njia moja wapo ya kuboresha penzi lako kwa umpendae.

2. ZAWADI ZINAJENGA KUMBUKUMBU KATIKA MAHUSIANO:


Umuhimu wa pili wa zawadi katika mahusiano ni kujenga taswira ya kumbukumbu kwa rafiki, jamaa au mpenzi wako, fahamu kuwa unapompa zawadi inakusaidia wewe kujijenga katika mawazo yake na endapo kama itatokea mkaachana nae basi pindi atakapokuwa anaziona zawadi zako zitamfanya akukumbuke kwa mengi na atahisi kama kuachana nawewe kwake kunatofauti na atajihisi kupoteza vingi toka kwako na kamwe kumbukumbu yako kwake haitofutika kila azionapo zawadi zako.

Soma:Tabia 30 za mwanamke anaeweza kukufaa katika maisha yako
 

Mpenzi msomaji wa ukurasa huu napenda nikushauri juu ya zawadi unazotakiwa kumpa mpenzi, rafiki, ndugu au jamaa yako jitahidi pindi unapohitaji kumnunulia zawadi tafuta zawadi ambayo itadumu kama vile nguo, card, maua n.k. Isiwe zawadi ya muda mfupi isiyotunzika kwa mfano hela jua atazitumia zitaisha utakuwa hujajenga misingi imara wa mahusiano.

KUMBUKA:
Simaanishi kuwa usimpe 
rafiki, ndugu au jamaa au mpenzi wako hela hapana ila inabidi ufahamu kuwa pesa hutumika katika kukidhi mahitaji na sio katika kuboresha mapenzi.