Featured Posts

July 15, 2017

Njia kuu nne za kuweka akiba.

KUWEKA AKIBA
Taifa lenye akiba ya kutosha,uchumi unakuwa imara muda wote hata pale majanga yakitokea laweza stahimili yote hayo pia mtaji mkubwa kwa taifa kuwekeza kwa miradi mikubwa, mtu kuweka akiba nayo ni muhimu sana kama vile kwa taifa, inaaminika watu kisaikologia ya fedha mtu hupenda tumia sasa kuliko kusubiri baadae ambapo ingeongeza faida na thamani zaidi, fedha ni kitu ambacho kipo.

Tu kwa muda kama mtu aliyekuwa nayo sasa  akishindwa kuidhiti leo kesho hatokuwa nayo, Jambo mtambuka hapa ni je kwa nini niweke akiba au niwekeze kwa jambo lingine? Yote yanaweza kuwa majibu sasa, Ningependa ongelea  njia mbalimbali za kuweka akiba zikitumika zinaweza kukuletea kwa karne hii,japo ni kwa afrika kuweka akiba ni swala sugu kwa walio wengi hii ni kutokana na uwezo mdogo wa kuthibiti fedha kisasa na kibiashara  pia elimu juu ya jambo hili  haijafika au kaa vizuri katika upande wa ubongo iliyo wazi.

Zipo njia ambazo ni nzuri zikitumika kwa kuweka akiba kwa faida itaongeza maendeleo ya wengi, hizi ni baadhi ya hizo njia:
   
(i) Kununua fedha za kigeni.

Mara nyingi fedha za kigeni mfano dollar,euro,pound,na fedha kutoka  bara Asia kama fedha ya saudi Arabia huwa zinapanda dhamani ukilingina na fedha ya tanzania ,mfano deo alinunua dollar  moja mwaka jana novemba kwa tsh 1300, amekuja kuuza dollar february 24  kwa tsh1539,hapa deo amepata faida ya tsh 239,mathalani umenunua dollar 5000,ni faida  itakuwa kubwa tu,faida ya hii njia ni moja inapunguza kukwepa kuwa na lundo la fedha nyingi ,pia kutokuwa na haraka yakutumia kuendelea kuiweka akiba,na pia mfumuko wa bei unakupa wewe faida,pamoja na mara kadhaa unapopenda kusafiri nje ya nchi kesho huwezi tabiri fedha za kigeni zinapanda thamani mara nyingi hivyo kama kipindi cha nyuma ulikuwa umetunza fedha nyingi za kigeni hapa wewe huwezi athiriki maana huna haja ya kununu fedha wakati unazo tayari tena kwa bei ghali.
   
(ii) Simu benki pesa.

Huu ni mfumo upo afrika mashariki,makampuni kama vodafone kupitia huduma ya M-Pesa  ilifanya mapinduzi ya benki pesa kenya,kisha huduma hizi zikaenea nchi kama Tanzania,Rwanda nk,hii ni huduma ambayo huu mrahisishia mteja ata kama akiwa mbali na benki hivyo kumfanya iwe ni kwa unafuu wa kuokoa muda na gharama za usafiri mteja anaweza weka akiba muda wowote ule,pia hata kama mteja huweza kuyakabili dharura inapotokea kwa kufanya transaction  kupitia simu hii ni huduma mfano kununua umeme,kulipia huduma ya kingamuzi,kulipia matibabu nk.

(iii) kuweka akiba kwa kutukia Benki na taasisi za nyingine za kifedha.

Hizi husaidia sana kuhamashisha huduma za kuweka akiba,mfano kuna  za kumwekea akiba za watoto wadogo,kuweka akiba za  amana,pia hizi zote huduma husaidia kuleta  mabadiliko,pia  taasisi ndogo ndogo za kifedha nazo zimekuwa mstari wa mbele kuhamashisha kuweka akiba kwa watu wa kipato cha chini kuanzia kiwango kidogo sana,matokea ya hizi  huduma ni kuwezesha watu kuwa na fedha za kukabili dharura,kuwa na mitaji mikubwa ya kibiashara,na hatimaye kuleta maendeleo makubwa nchini

(iv) kumkopesha mtu na kurudisha kwa riba.

Siku hizi huu mfumo umeenea sana ,haswa maeneo ya mjini na vyuoni,watu baada kuzidi kukua sana  kiuelewa wamebadili mwelekeo kutoka kumkopesha mtu pasipo riba,hadi kukoposha kwa riba,hii ni kwa sababu thamani ya fedha ya mwezi au wiki hii  ni tofauti na ya mwezi au wiki lijalo.Tatizo lililopo ni hakuna maandishi ya kukopeshana kwa walio wengi sababu kuu ni utu,hili ni tatizo,mwanadamu tabia yake kuu ni kubadilka badilka,kama huna maandishi ya kukopeshana itakuwa ni ngumu kupata pesa zako

Kuwekea bima mali zako na biashara yako,Hii ni njia amabayo ni muhimu sana  maana hamna mtu anaweza zuia majanga amabayo ni asili au yakawaida hivyo bima hapa inasaidia sana siku ukipata ajali ya biashara kuibiwa,kuungua,nk kulingama na bima uliyoweka.

Maendeleo ya mtu mmoja mmoja ni maendeleo ya taifa,taifa lenye akiba ya kutosha ni taifa imara,na wanachi wenye akiba kwa njia mbalimbali kama nilivyoorodhesha hapo juu ni watu wenye maisha ya uhakika,dharura zote wanaweza kukabili,mitaji mikubwa ya biashara  inatokea hapa.Kuna sera zenye mvuto wa kuhamashisha kuweka akiba ni jambo la msingi tuanze leo kuweka akiba.