July 29, 2017

Nchi 10 zenye amani zaidi duniani.

1. Iceland
Uharifu ni kama hamna kabisa katika nchi hii,(1.8 per 100,000) ni nchi yenye watu walioelimika

2. Denmark
Wadenmark inasemekana kuwa ni watu wenye furaha zaidi kuliko mataifa mengine yote duniani.Twakwimu zinaonyesha motisha za wafanyakazi zipo juu sana na kuna mfumo mzuri wa ustawi.Kodi zao zipo juu lakini fedha wanazotoa zinatumika kweli kwa ajili ya matumizi sahihi na kwa utaratibu mzuri.

3. New Zealand
Nchi yenye watu wachache, watu wa nchi hii ni wakarimu na wanapenda kufurahia mazingira na kujihusisha katika michezo

4. Austria
Nchini Austria kijana wa miaka 16 anaruhusiwa kupiga kura ila pombe inaruhusiwa kwa watu waliofikisha miaka 18 na kuendelea.Ni nchi yenye gharama nafuu na uhalifu katika nchi hii upo viwango vya chini sana.

5. Switzerland
Siri ya nchi hii kuwa na fuaraha na jamii yenye afya ni mamlaka za nchi hiyo kuweka nguvu zaidi katika kuwapa watu wake elimu bora, huduma bora za afya na kuwaajiri sana watu wake.

6. Japan 
Ni nchi ya watu waliostaharabika sana na ina miundo mizuri ya usafirishaji.Wajapan wanafanya kazi sana ila wametengeneza nchi yao na kuwa na amani na iliyoendelea sana kiteknolojia.

7. Finland 

Nchi hii haina rushwa na matabaka baina yao ni kwa kiasi kidogo sana. Inafanya vizuri katika usawa wa kijinsia.Pia ina mfumo mzuri sana wa elimu duniani.

8. Canada 
Ni nchi inayolipa vizuri kaya zake kwa wastani wa $28,000 kwa mwaka, na pia ina nafasi nzuri za kazi. 

9. Sweden 
Ni moja ya nchi ya kiscandinavia zilizo katika nafasi ya juu ya amani, Sweden inajulikana kwa wingi wa barafu na kipupwe cha mda mrefu. Maisha bora na mfumo wake mzuri wa ustawi wa jamii unaifanya Sweden kushika nafasi za juu.

10. Norway 
Norway ni miongoni mwa nchi zenye usalama, idadi ya wafungwa katika nchi hiyo ni ndogo. Pia ni nchi inafanya vizuri katika maswala ya afya na furaha.