July 27, 2017

Throwback: Hii hapa barua ambayo Askofu Kakobe alimwandikia Mh. Jakaya Kikwete.

Wakati hali ya sintofahamu katika duru za siasa na mambo ambayo hayakutarajiwa katika chama tawala (CCM) kama vile kumeguka, kutokana na baadhi ya watu wenye ushawishi mkubwa kama vile Mh: Edward Lowassa kukihama chama hicho tawala (CCM) na kuleta mpasuko mkubwa.

Jambo hili si la bahati mbaya au ghafla kama wengi wetu tunavyodhani au tunavyoona. Nakumbuka tarehe 10 machi 2014 Askofu mkuu wa kanisa la FGBF Zachary Kakobe alimuandikia barua ya wazi Rais wa Tz mh Jakaya Kikwete iliyokua na kichwa cha habari:-


UJUMBE WA WAZI WA MUNGU KWAKO NA KWA UMMA WOTE WA TANZANIA.
Swala/chanzo kilichompelekea Askofu mkuu Zachary kakobe kuandika ujumbe huu mzito ni baada ya serikali ya chama cha mapinduzi kutupa kapuni majina ya wapentecoste waliopendekezwa kua wawalikishi katika bunge la katiba, Hivyo kufanya taasisi hii kubwa ya kipentecoste yenye waumini mamilioni hapa Tanzania kukosa hata mtu mmoja wa kuwawakilisha hali ya kua hata waganga wa kienyeji walipata wawakilishi.Binafsi ninajiridhisha kua hilo ni moja tu kati ya maovu/upuuziaji ambao umekua ukifanywa kwasababu wameamini wanauwezo wa kufanya lolote wanalojisikia kwa maslahi binafsi na chama chao.

Ninaamini askofu Zachary Kakobe angesema aorodheshe mambo yote katika ile barua kingegeuka kua kitabu na si barua tena.
Sisemi haya kwasababu ni CCM wamefanya la hasha…waraka huu si wa mlengo wa kisiasa au wa kukitetea/kukiumiza chama chochote.

Lengo langu ni kuuweka ukweli wazi na ieleweke kwamba haya ni mavuno ya mbegu iliyopandwa.


MUHIMU:
Katika barua ile ya Askofu mkuu mzee wetu Zachary Kakobe ulikua ni waraka wa Mungu alioupata baada ya kuingia katika maombi ya muda kadhaa baada ya swala lile kutokea 
katika barua ile ujumbe hasa ambao ulikua ndio muhimu kwa Rais na chama chake pamoja na umma mzima wa Tanzania uliandikwa kwa maandishi ya rangi tofauti ili kuupa uzito na umakini ulioustahili,ujumbe huo ulikua kama ifuatavyo.


NANUKUU:
Chama unachokiongoza kimekua kikifurahia umoja na mshikamano kwa miaka mingi,Hata hivyo katika miaka ya hivi katibuni umoja na mshikamano huo umechukua sura mpya na kua umoja wenye malengo mabaya kinyume changu.


Kama umoja ule wa watu wa kale waliojenga mji na manara wa babeli kinyume changu na hivyo wakanifanya kuwachafulia usemi wao ili wasisikilizane wao kwa wao na nikawatawanya usonivpa nchi yote wakiwa makundi tofauti tofauti. Vivyo hivyo chama chakokimeiongoza serikali unayoiongoza kufanya mambo mengi yaliyo kinyume nami na kudharau wingi wa wema wangu kwenu na uvumilivu wangu msijue kua wema wangu kwenu umekua na lengo la kuwavuta mpate kutubu.

Kwa kadri ya ugumu wa mioyo yenu isiyo na toba sasa mmejiletea hukumu (Warumi 2:4-6)
Sasa ninawachafulia usemi watu wote katika chama chako, kwenye nafasi mbali mbali za uongozi ili msisikilizane ninyi kwa ninyi kuanzia sasa katika vikao vyenu mtafarakana na kutokusikilizana.

Mafarakano hayo yatadhihirika hatua kwa hatua na kuongezeka viwango tofauti tofauti na yatafikia kilele chake mwaka kesho 2015 ambapo kutakua na mafarakano makumbwa ambayo hayajawahi kutokea tangu chama chenu kipate kuwapo.

Nguvu za dola,nguvu za miungu ambazo baadhi yenu mnazitegemea, nguvu za fedha, hekima ya kibinadamu; Vyote hivyo havitaweza kuzuia mafarakano hayo.Kwa tendo hili mtajua kua alie juu ndie anaemiliki katika ufalme wa wanadamu na humpa amtakae awae yote; na wale waenendao kwa kutakabari yeye huwadhiili.”

Katika barua ile ambayo naweza kuiita ya kinabii iliambatana na mambo muhimu matatu(3)
1:Ujumbe wa wazi kuelezea tatizo
2:Madhara ya tatizo/uovu ambao umekua ukifanywa
3:Jinsi gani watazuia madahara yasitokee(TOBA)

Hayo ni mambo muhimu sana ambayo askofu Mkuu Zachary Kakobe aliyaorodhesha katika waraka ule.
Swala la toba ya kweli juu ya chama hicho na viongozi wake ndio ilikua njia pekee ya kuzuia haya tunayoyaona leo yasiyokee…!
Lakini kwasabau walipuuuza kama ambavyo wamekua wakifanya basi si ajabu kuona haya leo yanatokea, na pengine yapo mengine makubwa zaidi ya haya yanakuja.


WAZO KUU LA MWANDISHI WA MAKALA HII (WAZO LANGU)


Kumekua na mitazamo na hisia tofauti sana juu ya haya yanayotokea hivi sasa katika nchi hii. 
Lakini barua hii ya ya Askofu Kakobe ni kama watu hawaioni hivi.
Ninachokifahamu angesema kitu ambacho hakijatokea mitandao yote ya kijamii zingejaa habari zake na watu kusema kila mtu kwa namna anavyojisikia kusema.


Lakini kwa swala hili ukiliangalia kiimani ninapata jibu la moja kwa moja kwamba Mungu yuko kazini na taifa la hili…! Sisemi haya eti kwasababu lowasa kajiunga na ukawa au kwa sababu ya hali ya kisiasa inavyokwenda …La hashaaa!
Ila kiuhalisia mambo yaliyokua yameshindikana kwa muda wa zaidi ya miaka 50 leo kuwezekana kirahisi ndani ya sekunde kadhaa.
Kwa mtu mwenye jicho la imani ni lazima tujue kwamba Mungu analiandaa taifa hili na majira mapya.
Kwa namna yeyoye ile ambayo itatokea au kwa mtu yeyote atakaye tumiwa ilikua ni lazima neno la Mungu litimie na limekwiaha kutimia hata sasa.WITO WANGU KWA KANISA LA TANZANIA
Kama kuna wakati kanisa linatakiwa kua makini sana ni huu,Nyakati kama hizi ambazo mambo yanayofanyika katika ulimwengu wa roho yanaanza kujidhihirisha kwenye macho ya nyama ni wakati muhimu sana kwa kanisa kuingia magotini na kuomba kuliko kuanza kusimama na wanasiasa fulani eti kwasababu kuna muelekeo fulani unaonekana.
Kama Mungu ameweza kufanya haya yanayoonekana leo kutokea basi pia ni vizuri kujua anauwezo pia wa kuugeuza hata huo upepo tunaouhisi kua ni sahihi kuelekea mahali pengine kama jinsi alivyoufanya moyo wa farao kua mgumu.Ninaomba niseme kwamba hali ilipofika sasa si nzuri hata kidogo na hatima ya nchi hii ipo mikononi mwa kanisa.Tuna muda mchache sana wa kukaa magotini na kumsihi Mungu juu ya hili taifa ila cha ajabu hata kanisa nalo wanaendeshwa na upepo.
Unaweza ukafurahia au usifurahie ukweli huu ila kwa hali ya kisiasa ilivyo sasa hakika wakati wa uchaguzi lolote linaweza kutokea hasa kama kanisa litasahau kusimama katika nafasi yake na kuendelea kufuata upepo huu
Kama amani inatengenezwa basi na vita hutengenezwa pia.


Mambo yalipofika hapa ni dhahiri hii si akili wa kibinadamu inayoamua, Haya ni maamuzi ya ulimwengu usioonekana (VITA YA ROHONI HUPIGANWA ROHONI)
Nalisihi kanisa la Mungu
1:Jiandikisheni kwa wingi
2:Tunzeni vitambulisho vya mpiga kura
3:Turudini magotini tukakimalize tilichokianza
SHALOOM SHALOOM SHALOM
NA IWE SHWARI KUU JUU YA TANZANIA