July 21, 2017

Mambo 4 ya kuzingatia katika wazo la biashara.

1. Tambua Changamoto.
Kabla hujaanza jambo lolote lile ,kwanza fanya utafiti wa kutosha ,juu ya wazo lako ambalo ungependa kulitumia ili liweze kukuletea faida,changamoto hizi zipime katika Nyanja Kisheria,kimtaji vinavyoweza kuzuia wazo la biashara yako,aidha kwa kutambua vikwazo ,kwa kutofautisha biashara yako na nyingine ambazo zinakuzunguka,kabla ya kuanzisha ya kwako.


2. Orodhesha mahitaji ya wazo lako.
Wazo la biashara mara nyingi lazima liwe tofauti na wazo jingine au biashara nyingine,zingatia mahitaji ya wazo lako kwa kuangalia upekee wa biashara yako,huduma utakayokuwa unaitoa kwa kiwango gani,walengwa ni wakina nani,tambua jinsi ya kumvutia au sababu za kumfanya mtu avutike katika biashara yako badala ya bidha na huduma nyingine zilizopo katika mazingira yanayo kuzunguka.


3. Mbinu za kukuza Biashara yako.
Kuwa na mikakati na malengoni jinsi gani utaweza kuikuza biashara yako,kwa kutafutia njia sahihi na jinsi gani mteja wako au walengwa wa biashara yako wataweza kuipata huduma yako ili ikue na kusambaa mahali tofauti na kupata masoko,changanua ni jinsi gani utawafikia wateja wako,ni kwa vipi hao wateja wako watajua juu ya biashara na huduma yako.Utasambazaje bidhaa yako na kuwafikia walengwa wako.Haya ni maswali ambayo utapaswa kuyajibu ndani ya wazo lako la biashara yako ambayo umelenga kuifanya aidha ukiwa mjasiliamali binafsi au katika makundi.

Mbali na haya,jiulize katika Nyanja nyingine pia,katika wazo lako ,fanya makadirio ya idadi ya makadirio ya wafanyakazi unaowahitaji kufanyanao biashara yako, Unahitaji ufanye nini ili biashara yako ipate faida na itachukua muda gani kuwa na faida?mchanganuo huu utakusaidia kujua kiasi gani utaweza kutumia katika biashara yako na kiasi utakachokua unaingiza,huku ukiwa na mipango na matajio yako ya kipato unachokipata na matumizi yako kwa kipindi ambacho unaweza kujikadilia aidha kwa miaka miwili au mitatu.
Hili uweze kufanya haya yote ni lazima uwe na mtaji, nakatika wazo lako la biashara lazima ujiulize kwa vipi utaweza kupata mtaji,kuweka akiba benki au kuomba mkopo kwa kuzingatia biashara yako inahitaji ghalama ya kiasi gani ili uweze kuendesha bishara yako na kukua.4. Ufanisi wako katika Biashara.
Hapa kuna vitu vingi ambavyo unatakiwa uwe navyo ambavyo vitakua msingi wa kukuongoza kufikia malengo ya kazi ambayo unataka kuifanya,pamoja na kuwa na wazo la biashara,kwanza fanya tathmini ya kiwango cha elimu ulionayo na uzoefu unaorandana na wazo lako la biashara kwa wakati huo ukizingatia wadau wanahusiana na wazo lako la biashara kama unataka kuingia katika mjasiriamali.Tathmini hii itakuwezesha kwanza kujuana na watu ambao watashabiiana na wazo lako la biashara ambao watakua na network(mtandao) kuweza kupata masoko.
Orodhesha wataalamu ambao utawahitaji kufanya nao kazi ambapo wewe huna uwezo nako ili,kuanzisha ,kufanikisha na kuendesha biashara yako,fanya tathimini ya kiwango cha fedha ambacho utaweza kukitumia katika kuendesha biashara yako.
Kwa kuzingatia haya ndani ya wazo lako la biashara,kuna uwezekano mkubwa wa kuanzisha na kuendeleza biashara yako,msingi wa mtaji utategemea mambo manne ambayo ni kmuhimu katika biashara au mradi ambao umedhamilia kuuendesha,au biashara unayotaka kuiendesha.
Swala la ajira kwa vijana linahitaji ubunifu,kujitoa na kukubalina na changamoto utakazo kuwa unakabiliana nazo,lakini vijana wanafeli kwa kutegemea baada ya elimu yao,mawazo yao ni kufanya kazi zenye kipato kikubwa kwa wakati mfupi,lakini kumbe kwa kuanzisha biashara kwa kutumia wazo lako ni vema zaidi kwakuwa utakua unafanya kwa moyo na kwa kujitoa kwa kujua kuwa chochote kitakachotokea kinahatari ya kuangusha wazo na biashara uliyoianzisha.