July 22, 2017

Matendo ya chuki yanakuathiri we mwenyewe kuliko yule mtu unayemchukia.

Chuki ni pale unapowatafsiri watu wengine VIBAYA kwa sababu ya mtazamo mbaya ulionao juu ya watu hao, na uko tayari kufanya chochote kile kuhakikisha watu hao hawafanikiwi, hawafurahi, hawaendelee katika elimu ama chochote kila wanachokifanya.

Fatana nami katika story hii ya Bwana mmoja nchini Marekani aliyekuwa na chuki na jinsi chuki ilivyomuathiri.

Siku moja nchini marekani mzungu mmoja aliingia kwenye mgahawa na kukuta kuna kijana mmoja mweusi amekaa kwenye Kona ya mgahawa huo.

Akaingia ndani na kumwagiza muhudumu awape watu wote chakula kasoro yule kijana mweusi na pesa atatoa yeye.

Muhudumu akagawa chakula kwa watu wote kasoro yule mweusi na kisha akaenda kwa yule mzungu kuchukua malipo.

Yule mzungu akalipa pesa huku akimtizama yule mweusi.

Yule akamtizama kwa sura ya bashasha na tabasamu kisha akamwambia Yule mzungu asante.

Yule mzungu akachukia inakuwaje yule mweusi anafurahi baadala ya kukasirika..!

Akamuita muhudumu na kumwambia wape vinywaji BURE Mimi ndio nitalipa kasoro yule mweusi.

Muhudumu akawapa vinywaji wote kasoro yule mweusi.

Yule jamaa akalipa pesa ya vinywaji huku akimtizama yule kijana mweusi, cha ajabu yule kijana mweusi akaonyesha tabasamu kubwa zaidi kuliko mwanzo na kusema ahsante sana.

Yule mzungu akamfuata muhudumu na kumuuliza vipi huyu kijana mweusi ni mwendawazimu? mbona nafanya yenye kumkera lakini yeye anafurahi na kusema ahsante.

Muhudumu akamwambia huyo ndio mwenye mgahawa HUU..

Mafunzo: Tujifunze kuondoa chuki mioyoni mwetu kwani Ubaya umfanyiao MTU huenda ikawa sababu ya kunufaika kwake na ikawa njia ya kuanguka kwako.