July 29, 2017

Hizi hapa ndio dalili za mimba.

Kwa wale wanawake ambao wana kawaida ya kwenda hedhi kila mwezi, dalili ya awali na ya uhakika  ya ujauzito ni kukosa siku. Wakati mwingine wanawake ambao ni wajawazito na  wanapata siku kipindi kifupi sana, hutoka damu kidogo tu. Baadhi ya ishara na dalili nyingine za awali za ujauzito ni hizi hapa chini. Kila mwanamke ni tofauti na si wanawake wote watakuwa wataona  dalili hizi zote.

Kuhisi kuumwa - baadhi ya wanawake hujihisi kuwa wanaumwa. Wengi huhisi kichefuchefu na kutapika hasa nyakati za asubuhi.

Kuhisi uchovu-wanawake wengi hujihisi uchovu na mwili kulegea. Hii hufanya wanawake wapende kulala. Mabadiliko ya homoni yanayotokea wakati huu ndio kiini ya matatizo haya.

Kuumwa maziwa-baadhi ya wanawake hujaa na kuumwa maziwa.