July 27, 2017

Fahamu ukweli uliojificha juu ya samaki nguva anayefananishwa na binadamu.

Mnyama aina ya Nguva ambaye watu wamekuwa wakimwelezea kwa namna tofauti tofauti na endapo mazingira ya bahari yataendelea kuchafuka kuna uwezekano wa kiumbe hicho kutoweka.

Hii habari ya kiumbe kinachoitwa nguva ni kweli yupo ila ni samaki tuu na sio kweli kuwa ni nusu mtu nusu samaki!. Picha zote za kiumbe hicho unazoziona ni za kutengeneza, yaani ni hoax. 

1. Nguva ana rangi ya kijivu na umbo la mwili wake ni nyofu na uso wa umbo la nguruwe. Awapo katika maji hutoa kichwa chake juu ya maji kuvuta hewa kwa kutumia mashimo mawili ya pua yaliyopo upande wa juu wa kichwa chake.

2. Nguva ni mnyama anayezaa na kunyonyesha kama walivyo wanyama wengine na wakati akinyonyesha husimama na kukumbatia mtoto wake hali inayoweza kumfanya mtu aliyemuona kudhani kuwa ni mtu.

Isikupite hii: Watoto wanaolaziwa wakiwa na uzito mdogo hawata oa - utafiti.

3. Mnyama huyo huzaa kila baada ya miaka mitatu au saba na huzaa mtoto mmoja pekee hivyo nguva anahitaji kuhifadhiwa kwa kutovuliwa kwa manufaa ya kizazi kilichopo na kijacho ima kuweka kwenye maeneo tengefu.

4. Mtoto wa mnyama huyo anapozaliwa huwa na kati ya kilo 153 hadi 200, wakati nguva mkubwa huwa na kati ya kilo 400 hadi 1, 000 huku chakula chake kikuu kikiwa ni majani

5. Alikuwa akionekana Dar es Salaam, Kimbiji, Buyuni, lakini sasa haonekani tena kwani ni mnyama mwenye aibu sana na anapogundua kuwa maeneo alipo kuna binadamu huamua kuhama na kwenda mbali zaidi kwenye utulivu.

6. Kuna simulizi za ajabu ajabu kuhusu huyu samaki; kwa mfano wanasema kwamba mvuvi akimvua lazima kwanza afanye naye tendo la ndoa kama tambiko.)