Featured Posts

July 23, 2017

Godwin Ndugulile, Mtanzania aliyerudi TZ toka Marekani na teknolojia ya ajira za maelfu

Swala la usafiri hasahasa kwenye miji mikubwa ni hitaji la kila siku pale ambapo una ishu zako za hapa na pale, ishu kubwa pia kwenye miji mingi ya Afrika ni kulipia bei kwa mfumo wa maelewano pale unapochukua Tax, Bajaji au Bodaboda kero ambayo wengi wameilalamikia.

 Godwin Gabriel Ndugulile ni Mtanzania aliyeondoka Tanzania kwenda kusoma Marekani akiwa na umri wa miaka 17 ambapo baada ya kuishi kwa zaidi ya miaka 20 kwenye taifa hilo lililoendelea kiteknolojia, ameamua kurudi nyumbani Tanzania kuleta teknolojia ili tuishi kirahisi kama Marekani.


 Akiwa kule Marekani alianzisha kampuni inaitwa MOOVN ambayo inatumia mfumo wa Teknolojia kutoa huduma ya usafiri kirahisi na ndivyo hivyo inafanya kazi Tanzania, kampuni hii haimiliki gari lolote ila inachofanya ni kama wewe una gari lako unakwenda kuwaona na kujisajili.


 Baada ya kujiandikisha utakua na uwezo wa kulifanya gari lako, Bajaji au Bodaboda kuwa TAX bila kuchorwa mstari, kuwekewa bango la tax kwa juu au kukaa kituoni kusubiria abiria, teknolojia yao rahisi itakuwezesha kupitia simu yako ambapo hapohapo ulipo utaona abiria wanaohitaji huduma ya usafiri wakituma ombi kupitia teknolojia uliyopewa na itakuonyesha abiria anapotaka ukambebe na anapotaka umpeleke pia abiria ataona nauli aliyopangiwa.

 Teknolojia hii ina usalama zaidi ambapo wewe abiria kabla ya gari kukufikia, utawezeshwa kuona taarifa zote muhimu za Dereva na gari linalokuja kukubeba zikiwemo namba za gari, aina ya gari, picha ya dereva na mawasiliano sababu Dereva amesajiliwa na kufata kanuni nzuri ambazo MOOVN wameziweka kuhakikisha usalama wa abiria unakua mkubwa hivyo hata ukisahau kitu kwenye gari utakipata bila tatizo


               Mwanzilishi wa MOOVN, Godwin Gabriel akiwaelekeza Madereva via UrbanGKZ

Vilevile Dereva ataonyeshwa picha ya abiria anaekwenda kumbeba, majina yake kamili pamoja na mawasiliano yake.


Kwa watu wote wanaoutumia mtandao wa Vodacom, wawe wamejiunga na vifurushi vya Internet au hawajajiunga….. hawatochajiwa gharama za Internet kwa kutumia APP ya MOOVN hivyo hiyo ni faida nyingine kubwa sana.

 Niliona Marekani jinsi ambavyo wenye magari wanatumia vizuri mfumo huu, mtu ana Discovery yake, Range Rover, Toyota au gari jingine na unakuta kaajiriwa mahali hivyo anafanya kubeba abiria pale anapokua free kwa kuwasha APP yake, uzuri ni kwamba MOOVN inaruhusu hata kama una Range Rover na unataka kubeba abiria na abiria akichagua kwenye menu kwamba anahitaji Range Rover, bei yake sio sawa na Bajaji.

Godwin amesema kampuni yake inashika nafasi ya tatu sasa hivi Marekani kwenye kampuni za usafirishaji wa aina hiyo akichuana na Ubber na Lift ambapo anaamini akiendelea kukaza zaidi atapanda zaidi ya hapo maana hakuwa kwenye nafasi hiyo kabla