July 22, 2017

Wanawake shtukeni! Sera za haki sawa chanzo cha kuvuruga ndoa zenu.

Zamani ndoa zilikuwa zinadumu sana. Lakini baada ya kuleta haki sawa tu ndoa siku hizi ni miezi miwili ishavunjika. Wanaanza kulala mzungu wa pili, kila mtu anajitegemea kama bachela na hata salamu hawapeani. Haya mambo ya haki sawa yaishie hukohuko Serikalini sio kwenye ndoa zetu.

Wewe unayetaka kuolewa au uliyepo kwenye ndoa, Mheshimu na Msikilize mume wako, Mfundishe, mshauri hata kumuelekeza.

Soma: Changamoto Kuu 6 Za Mahusiano Ama Ndoa.

Eti wanawake wa siku hizi wanafurahia kuona mume wake akiosha vyombo baada ya kula, akideki, akifagia, akipika na kubembeleza mtoto alale.

Wanawake wa siku hizi wanafurahi wakiona waume zao wakitangulia nyumbani saa 12 jioni huku mwanamke akija saa tano Usiku.

Wanafurahi kuona anaporudi kwa kuchelewa haulizwi alikuwa wapi, hataki kuona mwaume akigusa simu yake, hataki kupangiwa cha kufanya na mume wake.

Wanawake wa siku hizi wanapenda kuona waume zao wakitandika Vitanda na kuchomekea chandarua ikiwemo kupelekewa maji bafuni. Eti Mwanaume kama unashindwa kufanya hayo, tafuta mdada wa kazi afanye.

Hawa haki sana Wanawadanganya sana. Nia yao wanataka baadae waje wawasimiame katika kugawana vitu baada ya kutandikwa talaka na masikio yake.