July 22, 2017

Hizi ndio kampuni 3 za matangazo ya blog /website Tanzania.

Watu hudhani kwamba sisi ni wajinga. Katika mtazamo wa wengi, blogging ni kama utani.

Lakini ukipata nafasi ya kukaa chini na watu kama Bw. Millard Ayo mmiliki wa www.millardayo.com na Ayo Tv, Bw. Maxence Melo mmiliki wa www.jamiiforums.com ama Bw.Luca Neghesti mmiliki wa www.bongo5.com watakwambia blogging ni moja kati ya kazi zinazoingiza kipato kikubwa sana hasa katika ulimwengu huu wa sayansi na teknologia.

Bw. Michael Arrington hutengeneza kiasa cha Dollar 500,000/= - 800,000/= kwa mwenzi mmoja tu sawa na Shilingi 1,120,747,808 - 1,793,196,493 za Kitanzania, kutokana na kazi hii ya "Blogging" ambayo wengi huona kama matani.  

Leo sina mengi ya kusema lakini napenda nikutiiye moyo wewe kama blogger mchanga, juhudi zako, kuamka kwako mapema na kulala masaa yameenda sio bure, fanya kazi kwa bidii ukiwa na malengo.

Nenda kwa bloggers wakubwa waulize maswali mbalimbali lakini pia tumia google kusoma njia na mbinu mbalimbali za kukuza blog yako, kuongeza ranking kwa google search n.k.

Hizi hapa ni kampuni 3 za matangazo ya blog/websites hapa Tanzania.