July 27, 2017

Je uzuri na fedha vina nafasi katika mahusiano?

Tajiri na fedha zake asipopendwa huwa katika mateso na kukonda wakati ana kila kitu. Upendo wa kweli halinunuliwi kwa pesa.

Tabia ya asili huwa sawa na moto unaowaka kwenye pamba, ukitoa moshi ujue hakuna kilicho salama. Wapo watu wasiokuwa na upendo dhati, utakuta mtu anajifanya anakupenda ukiwa naye lakini mkiachana hana habari na wewe, hata kama mnakaa nyumba moja na kulala kitanda kimoja.

Isikupite hii: Namna 10 ambazo watu huwasaliti wenzi wao bila kujua.

Mtu anapoamua kutoka nje ya ndoa wakati ndani ana mke mzuri au mume wa ukweli, anayempa kila kitu, kuna mawili.

Kwanza
Huenda mwanamke aliyenaye alimtamani kutokana na sura na umbile lake na hakumpenda kwa dhati. Matokeo yake baada ya kumchoka, mwanamke huonekana hafai na hukaa naye kimazoea.

Upande wa mwanamke, naye huenda amekwenda kwa mwanaume kutokana na kujua ana fedha lakini anakuwa hana mapenzi naye. Hapo lazima atatafuta mpenzi wa nje ili afurahishe nafsi yake, kwa hiyo watu hawa kutoka nje sishangai.

Pili.
Tabia ya kutoridhika na mpenzi mmoja, watu wa aina hii huwa hawajisikii kuwa na mpenzi mmoja kwa muda mrefu, lazima atatafuta mtu mwingine. Vitu hivi vyote huwa vinawachanganya watu, hasa wale wanaoamini kuwa mwanaume anapokuwa na fedha au mwanamke anapokuwa mzuri, ni kila kitu katika mapenzi.

Isikupite hii: Baadhi ya mambo ya kufanya kuzuia kuumizwa na mahusiano.

Kumpata Mpenzi wa kweli ni kazi sana, hasa kumpata uliyemkusudia, basi muombe Mungu utakayemchagua naye awe kweli amekukubali, hata ukiwa mbali kila mmoja amlindie mwenzake heshima, kwa kutanguliza uaminifu mbele.