July 22, 2017

Jinsi ya kujitoa kikamilifu na kufanya maisha yako kuwa bora na ya mafanikio.

Hitaji lako la kwanza ambalo unatakiwa ulijue katika safari yako ya mafanikio ni kwamba, unahitaji sana kujifunza, kukua na kuendelea kufanikiwa yaani learn, grow and develop. Hilo ndilo hitaji lako la kwanza.

Kila wakati utahitaji ujue ni nini ufanye ili kuboresha maisha yako au ufanye nini cha zaidi ili hicho unachokifanya kikuletee matokeo makubwa na unayoyataka kwenye maisha yako leo na hata kesho.
 

Soma: Makubwa ya Magazeti ya TZ leo July 22.. Michezo na Hardnews


Unaweza ukaanza kuboresha chochote kile hata kwa kidogo sana. Unaweza ukaanza kuboresha tabia zako,  unaweza ukaanza kuboresha biashara yako au hata maarifa yako kwa kujisomea zaidi na zaidi kila siku.

Kuendelea kujitoa kikamilifu na kuboresha maisha yako linatakiwa liwe zoezi endelevu, kila siku jiulize, ni kwa namna gani unaweza ukafanya siku yako ikawa bora, ni namna gani unaweza kuboresha maisha yako kuliko jana?

Kufanya mabadiliko na kubadilisha maisha yako, ni jambo ambalo linachukua muda( Becoming a master takes time). Unatakiwa kujifunza na kuchukua mazoezi tena na tena ili kuwa mbobezi. Hakuna kikubwa ambacho utakachofanikisha kama usipofanya hivyo.

Hakuna mpaka wa kuboresha maisha yako, hakuna mpaka unaokuzuia wewe kukua kimafanikio. Kila iitwapo leo, endelea kuboresha maisha  yako kwa jinsi unavyoweza. Ukiendelea kufanya hivyo, uwe na uhakika utafanikiwa.

Jiulize kipi kinachokuzuia ili usifanye maisha yako yawe bora? Angalia usikwamishwe na hofu wala usikwamishwe na tabia za kuahirisha mambo kila wakati. amua kufanya kitu kitakachoyafanya maisha yako yaonekane ya maana.


 Isikupite Hii: Hili ndio limao kubwa zaidi duniani, lina uzito wa 5.2 kg (+picha)

Kama nilivyosema mwanzoni mwa makala haya, unahitaji sana kujifunza, kukua na kuendelea kufanikiwa. Kila siku jiulize, je, umejifunza nini? Je, kutokana na kujifunza huko kuna hatua yoyote unayopiga?

Kama hujifunzi elewa hautaweza kukua, wala hautaweza kufanikiwa. Maisha ya mafanikio ndivyo yapo hivyo, yanahitajji kuweka juhudi nyingi katika .katika kila eneo ili uweze kupiga hatua za kimafanikio.