July 31, 2017

Jinsi ya kupika kabichi kwa mayai.

Habari mdau wa jinsi ya kupika. karibuni tena katika jiko letu. Leo tuandae mboga ya kabichi. Mboga hii yaweza kupikwa kwa nyama, njegere, yenyewe tu kwa viungoviungo, na aina tofauti tofauti, lakini sisi leo tuipike na mayai, ni nzuri sogea karibu tuandae wote.

Mahitaji

 • kabichi 1
 • mayai 4
 • mafuta robo
 • vitunguu 4
 • nyanya 5
 • karoti kubwa 1
 • pilipili manga kiasi
 • chumvi kiasi kwa ladha

Jinsi ya kupika kabichi hatua kwa hatua

 1. Andaa kabichi ulikatekate kisha ulikoshe.
 2. libandike jikoni liive kidogo. kisha liweke pembeni.
 3. menya nyanya, kata vitunguu na karoti uviweke tayari kwa mapishi.
 4. bandika sufuria jikoni utie mafuta, yakipata moto tia vitunguu ukaange mpaka vibadilike rangi kisha tia nyanya ukaange.
 5. tia karoti kaanga kidogo, tia kabichi, pilipili manga na chumvi, vunja mayai uyapige uyatie. koroga hadi likauke, hapo linakua tayari.
Namna hiyo kabichi letu liko tayari, linakwenda sambamba na ugali, wali na hata pilau simbaya. Hivi karibuni mungu akipenda tutaandaa kabichi la njegere. karibuni sana