Featured Posts

July 30, 2017

Kanuni 7 za upatanisho katika mahusiano.

1. Watambue neno SAMAHANI halina jinsia

Aliyekosea ndiye aombe kusamehewa hili halijalushi ni mme au mke. Ubabe katika mahusiano si njia bora ya kumaliza tofauti zenu.

2. Tabia ya kususa susa siyo nzuri

Wengine wakisha tofautiana hususa wakidhani ndo wanatatua tofauti zao....wengine hususa kuongea, wengine hususa kula na mbaya zaidi wengine hususia hadi huduma ya kitandani ambao ndio nguzo muhimu katika mahusiano.

3. Ugomvi unaoanzia chumbani umalizikie kitandani

Ugomvi mliouanzia chumbani uishie chumbani hukohuko na usitoke nje. ........walio katika mahusiano wajitahidi kusikilizana na kutatua tofauti zao wenyewe na zaidi kitanda kiwe jukwaa la upatanishi na siyo vinginevyo.

4. Mmoja lazima akubali kuumia ili mwenzie apate amani

Jifunze kushuka( sometimes calm down) hii itakusaidia kurejesha amani katika mahusiano yako. Usipandishe sauti wakati unamwona mwenzio naye yuko juu na kajawa na hasira. Kwa kujishusha amani irarejea tu.

5. Acha mawazo ya kuachika

Huyo ni wako zaidi waza urejesho na siyo uharibifu. Mlikubaliana mkapatana na mkayaanzisha mahusiano. Usivunje mahusiano uliyoyajenga kwa muda na ghsrama kubwa kwa jambo dogo sana. Talaka haijawahi kumwacha mtu salama.

6. Samehe, Achilia na Mchukulie mwenzio

Hakuna aliye mkamilifu katika dunia hii.  Sisi wote tuna madhaifu (weekness) unapoona mahusiano yamedumu ujue hao wamefuzu kiwango cha juu cha kuvumiliana na kuchukuliana.

7. Jenga utaratibu wa kufanya ibada pamoja

Sote tunajua mpatanishi mkuu ni mwenyezi Mungu. Hivyo mnapounganisha mikono yenu kwa pamoja na mkamuita Mungu awasaidie hakika mnakuwa sehemu salama kuliko ukifanya vinginevyo. Mahusiano yanayomtegemea Mungu kamwe huwa hayateteleki.