July 15, 2017

Baadhi ya mambo ya kufanya kuzuia kuumizwa na mahusiano.

1. Sio mahusiano yote huishia ndoa. Mahusiano mengine yapo kama somo kwako, mengine ni ya msimu na machache ndio hua ya kudumu.

Kama mahusiano yako hayaendi kama unavyohitaji, usijiue, usijilaumu, wala usikate tamaa. Tambua kusudi lako na endelea na maisha.

2. Usimpe mwanamke au mwanaume moyo wako wote kabla hujampa Mungu wako. Mpende sana huyo mtu, lakini Mungu awe wa kwanza.

3. Usibabaishwe na uzuri wa mtu au utajiri alionao, kama huyo mtu ameshindwa kukuweka moyoni, uzuri wake au pesa zake haziwezi kukuweka pia.

4. Mapenzi pekee hayatoshi. Kuelewana, kuendana, busara, uvumilivu, uaminifu ni vya muhimu zaidi.

5. Pale dalili mbaya zinavyokua nyingi kuzidi dalili nzuri, ni vema ukajitoa mapema kabla hujaumia vibaya huko mbeleni.

6. Ni wazi kwamba, wivu uliopitiliza kiwango ni dalili tosha ya mahusiano kuvunjika.

7. Uaminifu kamwe hauombwi, haki yako kuupata, build it or show it!

8. Kamwe usimfananshe uliye naye na ex wako au na mtu mwingine. 

9. Mahusiano yenu yasiendeshwe na 'SEX' tu bali, kujaliana, upendo na mawasiliano.

10. Usimuoe au usiolewe nae kwa sababu umemuona kwenye nyumba ya ibada. Wengi wapo humo kwa madhumun mbalimbali. Usiangalie ni WAPI umekutana na huyo mtu, bali tizama ni mtu wa AINA gani.