July 28, 2017

Je unaijua saikolijia ya mwenzi wako katika mahusiano?

 JE UNAIJUA SAIKOLIJIA YA MWENZI WAKO KATIKA MAHUSIANO!!
Mambo haya yatakusaidia kutambua saikolojia ya mwenzi wako.

o        Mwanaume ni kiongozi wa familia
o        Mwanaume ni mlinzi wa mwanamke pamoja na familia
o        Mwanaume ni mfano wa kuigwa na jamii
o        Mwanaume ni mrithi wa Mungu

MWANAUME MWENYE ASILI YA MUNGU (MWENYE MAADILI MAZURI)

o   Ni mnyenyekevu wakati wote
o   Ni mvumilivu wakati wote
o   Yupo tayari kusuluhisha kesi yake na kuanza upya
o   Ni mwepesi kusamehe na kusahau
o   Ni mtu mwenye utu na anathamini utu wa mtu
o   Anajali watoto na mke wake pia
o   Hatakama atakuwa si muaminifu hujitahidi sana mke wake asijue

MWANAUME MWENYE ASILI YA DUNIA (ASIYE NA MAADILI MAZURI)

o   Ni mkorofi kupindukia
o   Hana utu wala kujali
o   Ni mtu wa lawama wakati wote
o   Hana hofu kwa chochote anachokifanya
o   Huhesabu makosa wakati wote
o   Hana maneno ya faraja kila wakati hulaani tu
o   Hana moyo wa kusamehe, siyo rahisi kesi yake imalizike kwa amani

1.  Kundi la kwanza linamtambulisha mwanaume mwenye anayefuata muongozo mzuri wa malezi kutoka kwa wazazi wake na pia sheria za dini ambazo zinamuandaa kuwa mwanaume mwenye majukumu ya mke na familia. 

Hivyo anapokutana na mwanamke asiye na maadili inamuwia vigumu sana kumbadilisha tabia na kama Mungu asipoingilia kati mahusiano haya kunaweza kumfanya mwanaume huyu asitamani tena kuoa au kuwa katika mahusiano maana huwaza kupenda na endapo atapata mwanamke mwenye maadili ndoa yao itakuwa nzuri sana kutokana na asili yao.

2.  Kundi la pili linamtambulisha mwanaume asiye na malezi na asiye jua nini wajibu wake kama mwanaume. Mwanaume huyu anakuwa katika hali kama hii endapo kwa upande mmoja wazazi wake walichangia katika malezi mabovu au wazazi walijitahidi sana kumfundisha lakini hakufundishika.

Mwanaume huyu anapokutana na mwanamke mwenye maadili au aliyefundishwa vizuri tangu mwanzo kuwa ipo siku moja atakuwa mke wa mtu itamuwia vigumu mke huyu kuchukuliana na huyu mwanaume na atahangaika sana kutaka kumbalisha lakini haitawezekana kwa kipindi kifupi tu. 

Itamlazimu kulipa gharama ya muda mrefu na kumtafuta Mungu zaidi kuliko kutumia akili zake mwenyewe.

3.  Katika makundi yote haya tunaweza kuona mwanaume uliyenae wewe yupo katika kundi gani na asili gani ili unapoanza kushugulika na kasoro unazoziona katika ndoa au mahusiano yako utambue mwanaume huyo asili yake ni nini na jinsi gani utaweza kusaidiana naye katika safari hii ya mahusiano au ndoa yenu.


MWANAMKE NI NANI KATIKA JAMII?

o   Mwanamke ni msaidizi wa mwanaume
o   Mwanamke ni taji ya mwanaume
o   Mwanamke ni mjenzi wa mji wake na nyumba yake
o   Mwanamke ni kipenzi cha watoto na mume
o   Mwanamke ni mwalimu wa familia
o   Mwanamke ni mshawishi wa tabia njema kwa jamii inayomzunguka

MWANAMKE MWENYE ASILI YA MUNGU (MWANAMKE MWENYE MAADILI)

o Hana haraka ya mambo
o Mvumilivu, mnyenyekevu, mtiifu, mkweli, anaheshima, anajituma, ana utu
o Yupo tayari kufanya suluhu na kusahau
o Yupo tayari kujifunza kutokana na makosa
o Ana mapenzi ya dhati nay a ukweli
o Anajali watoto na mume wake pia pamoja na jamii yote inayomzunguka
o Hayupo tayari kumsaliti mume wake hata kama sababu zote anazo.

MWANAMKE MWENYE ASILI YA DUNIA (ASIYE NA MAADILI)

o  Ni mkorofi
o  Hasira zake huwa karibu na za wazi wazi sana
o  Kinywa chake hutoa matusi na lawama wakati wote
o  Hukusanya makosa ya mume wake wakati wote
o  Huwa na upendo wa mtego, hana upendo wa dhati
o  Hupenda kupokea zaidi ya kutoa
o  Hulazimisha mambo yafanyike hata kama haiwezekani kwa wakati huo.

1.  Katika kundi la kwanza tunamuona mwanamke mwenye asili ya mungu ambaye hutambulika kama mwanamke shujaa mwenye maadili ya kuwa mke mwema na aliye andaliwa vizuri kuwa mke bora kwa mume na familia nzima.

Mwanamke huyu anapokutana na mwanaume mwenye asili ya dunia hujuta sana kwanini ameingia katika mahusiano na mtu huyu, inamuwia vigumu kuikabili tabia ya mwanaume huyu na kuona wanaume wote ni maadui na kama ikishindikana kupata msaada wa kumtoa katika eneo hilo basi hujikuta akibaki mnyonge na mwenye kilio wakati wote hatimae kutokuwa katika mahusiano tena. 

Anapobahatika kukutana na mwanaume ambaye ana maadili mahusiano yao huwa ya amani sana na hata ndoa yao huwa inadumu kwa kiasi kikubwa sana.

2.  Kundi la pili linamtambulisha mwanamke asiye na malezi na asiye jua nini wajibu wake kama mwanamke. Mwanamke huyu anakuwa katika hali kama hii endapo kwa upande mmoja wazazi wake walichangia katika malezi mabovu au wazazi walijitahidi sana kumfundisha lakini hakufundishika.

Mwanamke huyu anapokutana na mwanaume mwenye maadili au aliyefundishwa vizuri tangu mwanzo kuwa ipo siku moja atakuwa mume wa mtu itamuwia vigumu mume huyu kuchukuliana na huyu mwanamke na atahangaika sana kutaka kumbalisha lakini haitawezekana kwa kipindi kifupi tu. Itamlazimu kulipa gharama ya muda mrefu na kumtafuta Mungu zaidi kuliko kutumia akili zake mwenyewe.

3.  Katika makundi yote haya tunaweza kuona mwanaume uliyenae wewe yupo katika kundi gani na asili gani ili unapoanza kushugulika na kasoro unazoziona katika ndoa au mahusiano yako utambue mwanaume huyo asili yake ni nini na jinsi gani utaweza kusaidiana naye katika safari hii ya mahusiano au ndoa yenu.