July 6, 2017

Mimea huongeza hamu ya kufanya kazi zaidi ofisini - utafiti.

Mimea kwenye ofisi inaongeza mzuka kwa kufanya kazi kwa kiasi kikubwa, kwa mujibu wa wanasayansi.

Utafiti unaonesha kuwa fungu dogo la mimea ikiwa juu ya meza huongeza nguvu ya akili, kuridhika na kazi na afya. Mwanasaikolojia, Dr Craig Knight, aliyeongoza utafiti huo, amesema, “kuongeza mimea huwafanya watu wawe na furaha na wenye nguvu kazi.”

Utafiti huo wa kisaikolojia ulifanyika katika chuo kikuu cha Exeter huko Finland na kuhusisha wafanyakazi kwenye makampuni matatu.

Watafiti hao walibaini kuwa mimea michache tu mezani au ofisini ilikuwa na uwezo mkubwa wa kuongeza uzalishaji.