July 31, 2017

Naomba hii iwafikie wanaume wote, kwanzia baba mwenye nyumba na mme masuali pia.

Yuko cheap kwa sababu amekupenda wewe. Ni mnene kwa sababu amezaa. Ni mchungu moyoni mwake kwa kuwa ameumizwa vibaya kihisia.

Anakuboa kitandani kwa kuwa hana hisia na wewe tena. Umemsaliti mara milioni kidogo. Lakini bado hajaafikia kukuacha. Unamuona kama kituko yeye anakuthamini. Usimuhukumu bila kujua sababu.


Isikupite hii: Fahamu faida za pweza kwenye afya ya mwanadamu.

Mwanamke aliejeruhiwa kihisia ni hatari sana. Anasamehe haraka sana lakini hasahau kirahisi. Anataka ujutie makosa yako lakini wewe ndio kwanza unachochea kuni.


Maumivu yake hua hayaponi kirahisi, lakini amechagua kuishi na wewe hivyo hivyo. Anafake tabasamu, anafake orgasm, anafake kila kitu ili tu usimuache.


Atalia usiku kucha, lakini asubuhi ataamka na tabasamu utafikiri kila kitu kiko sawa. Lakini moyo wake unavuja damu. Kila mtu atafikiri yuko sawa lakini maumivu yake ndani ya moyo juu ya kusalitiwa na kudharauliwa na mume wake anayajua mwenyewe.


Ukweli au uongo?