July 18, 2017

Mazingira ambayo yanaweza kuchochea usaliti kwa wanandoa.

1. Kutokuvutiwa tena na mwenzi wako.

2. Kutokujali tena kuwa unaongezeka unene au kupungua kupita kiasi

3. Kubadilika mwonekano wako uliokuwa ukimvutia zamani mwenzi wako

4. Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa kwa mmoja wenu au kwa wote wawili. 

5. Kukosa hamu katika mavazi mazuri kwa ujumla, mtindo wa nywele na jinsi unavyoonekana. 

6. Kufanya tendo la ndoa mara chache sana miongoni mwa wanandoa.

7. Kukosekana kwa mawasiliano baina ya wanandoa.

Soma: Unamtambuaje Rafiki Mwenye Dalili Za Kuja Kuwa Adui.

8. Kushindwa kutengeneza hamu kuelekea tendo la ndoa.

9. Kushindwa kuendeleza yale yanayompendeza kila mmoja wenu.

10. Ndoa za kipindi cha likizo. Wanandoa wanaonana siku chache sana nyakati za likizo au sikukuu fulani fulani. (Hatari sana kwa ndoa hasa wanaume wana kiwango kidogo sana cha kuvumilia kuwa mbali na mwenzi wake na akabakia kuwa mwaminifu tofauti sana na wanawake.

11. Kushindwa kushirikiana chumba cha kulala au kulala vitanda mbalimabli, au kila mwanndoa kugeukia upande wake.

12. Kazi za kusafiri safari za mara kwa mara.

13. Kushindwa kumfikisha mwenza wako mara kwa mara katika tendo la ndoa.

14. Kufanya kazi pamoja mwanamke na mwaname (asiye mwenzi wako) kwa muda mrefu.

  • Kazi za kusafiri kwa pamoja mwanamke na mwanaume na kukaa hotel moja na mtu wa karibu asiye mwenzi wako. 
  • Kwenda kusoma pamoja kozi za nje ya mkoa wako au nje ya nchi na mtu asiye mwenzi wako.
  • Kwenda safari za kikazi au biashara pamoja na mtu asiye mwenzi wako.
  • Kufanya vikao au "counseling" katika vyumba vya hotel mwanamke na mwanaume asiye mwenzi wako.